Friday, April 3, 2020

VYAKULA 10 BORA VYA MAMA MJAMZITO NA FAIDA ZAKE

                                                                    ✍️DR.CHILO.
MwanaApp#online clinic

🌹🌹🌹Kwa ajili afya ya mama na mtoto ni muhimu sana, mwanamke anatakiwa apate chakula bora kilicho na madini yote kama vitamini na protini.

Mama mjamzito anatakiwa apate gramu 100 za protini kila siku.

👉👉Ifuatayo ni mlo kamili anaotakiwa apate mama mjamzito kila siku ya ujauzito wake kwa afya bora ya mama na kijacho.

❤️Nimeweza kukundalia vyakula 10 bora ambavyo mama mjamzito na mtoto wake wanastahili kupata.❤️

🌹1. Vyakula Jamii ya Kunde
Mbegu za makundekunde ni sehemu muhimu ya chakula kwa mama mjamzito kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha protini.
🌺🌺Kwa watu wasiokula nyama au wana uwezo mdogo tu kujipatia nyama mbegu za jamii kunde zinatosheleza mahitaji ya protini.
🌹🌹Hivi ni vyakula vya mimea kama Soya, Njegere, Karanga, Mikunde, maharage nk

🌹2. Mayai
Mayai mawili kwa siku husaidia kuupa mwili protini, vitamini A na madini ambayo husaidia kuzuia kupatwa na maradhi mbali mbali.

🌹3. Maziwa na vyakula vya jamii ya maziwa🌹

Maziwa ni muhimu kwa protini, calcium, vitamini na virutubisho vingi. Vitasaidia ukuaji wa mifupa na misuli ,  kukukinga na Fangasi wa kwenye uke,kusaidia usingizi na kusawazisha mapigo ya moyo.

🍌4. Matunda na Mbogamboga 🍏
Matunda ba mbogamboga vina vitamini vingi na madini  ambayo husaidia ukuaji wa macho ya mtoto, ngozi na mifupa.

🌹5. Nyama
Ya kuku, Nyama ya mbuzi  au ng'ombe (Maini) huwa na protini nyingi sana na husaidia katika ukuaji wa mwili wa mtoto hasa kwa mama mjamzito wa miezi minne

🌹6. Nafaka na vyakula vya Wanga
Vyakula hivi huipa mwili nguvu ya kufanya kazi na pia ukuaji wa mtoto tumboni. Vyakula hivi ni kama mahindi, mtama, mihogo, vyakula vya ngano kama mkate n.k.

🌹7. Parachichi🥑🥑
Ni matunda ambayo yana mafuta mengi maarufu kama fatty acid. Parachichi husaidia katika ukuaji wa ubongo, ngozi nyororo na ukuaji wa misuli ya mtoto tumboni.

🌹8. Mboga za majani🥦
Mboga za majani kama spinach, kabeji, mchicha na matembele. Mboga hizi zinafaa ziwe zenye rangi ya kijani iliyokolea kwa sababu hizi ndizo zenye virutubisho vya kutosha.
🥦🥦Mboga hizi zitampa mama na mtoto wake Vitamin A na B, pia virutubisho vitakavyosaidia mwili kupata protini ya kutosha, ukuaji wa mwili, na utengenezaji wa damu.
🥒Kutopata mboga za kutosha kunaweza sababisha mama kupata ugonjwa wa Anemia.

🌹9. Samaki
Mafuta yaliyomo kwenye samaki huwa na Omega fatty acids ambayo inasaidia ukuaji wa ubongo na macho ya mtoto.

🌹10. Maji🌺🌺
Maji ni muhimu kwa mwili kwa sababu inasaidia kwenye mmenyenyo na unyonywaji chakula na pia husaidia kuzia choo ngumu Maji pia huzuia uvimbe wa mwili na maambukizi ya mfumo wa mkojo(U.T.I)

🌹🌹MAMA k kula VIZURI uzae mtoto mwenye akili nyingiiiiiiiii🌺🌺🌺

No comments:

Post a Comment