MADHARA YA KULA UDONGO ,MKAA KWA WAJAWAZITO NA WATOTO.
✍️✍️haya Ni madhara kwa mtu anaetumia udongo au mkaa hii husababishwa na Upungufu wa madini,na vitamin mwilini .kitaaramu shida hii ya kula udongo,mkaa na karatasi na vitu vingine visivyo chakula huitwa Pica.
👩⚕️👩⚕️Pica hupunguza Uwezo wa mmeng'enyo wa chakula kufonza Virutubisho lishe na hivo kupelekea Upungufu wa virutubisho mwilini.
👩⚕️👩⚕️Baadhi ya pica ni sumu, hivo humweka mhanga wa matumizi ya pica katika hatari ya kudhurika.sio kila UDOGO umechanganyika na vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kukuzuru Afya yako.
👩⚕️👩⚕️Pica hua na uchafu wenye bakteria na vimelea vingine vya magonjwa hivyo huweza kusabisha maradhi ya homa ya matumbo, Kuharisha, Minyoo n.k
👩⚕️👩⚕️●Wakati wa kutafuna pica(udongo) huzalisha mchanga ambao hauwezi kufonzwa kupitia utumbo, badala yake hutolewa kama kinyesi na baadhi kurundikana katika kidole tumbo (Appendix) ambapo huweza kusababisha kuvimba au kuchanika (Appendicitis) kusababisha ulazima wa kufanyiwa upasuaji kuondoa kidole tumbo.
👩⚕️👩⚕️Kua mlaibu wa matumizi ya pica na kuhisi kua mgonjwa usipotumia pica yako yan usipokula udongo unaona Kama mwili haupo sawa .
👩⚕️👩⚕️Pica itamfanya mama Mjamzito kuzaa mtoto wenye Uzito mdogo .
✍️UFANYE NINI UKIPATWA NA HALI HII?🌹
🌺🌺Mweleze tabibu/daktari ili ufanyiwe vipimo vya madini joto/chuma.
🌹🌹Hakikisha unatumia dawa zote hasa za madini lishe pamoja na vitamini ulizoandikiwa kutumia.
👩⚕️👩⚕️Kama ni mjamzito au mtoto mdogo ambaye bado anahudhuria kliniki, hudhuria kadri ulivopangiwa bila kukosa ili kujua maendeleo yako na kupata ushauri zaidi kutoka kwa wataalamu wako wa afya.
🌹🌹jitahidi kufata Ushauri wa wataaramu wa Afya walio kwenye klinik yako.
✍️✍️MUNGU awabariki mama K Wote TUNAWAPENDA Sana.
No comments:
Post a Comment