Wednesday, April 1, 2020

UTUNZE UKE WAKO HIVI ,ZUIA BACTERIA VAGINOSIS


MAAMBUKIZI UKENI (BACTERIAL VAGINOSIS)
✍️✍️DR.CHILO
tatizo hili la maambukizi ukeni ni hali inayotokea mara nyingi kwa wanawake.hali hii inasababishwa na kuvurugika kwa mazingira rafiki kwa wadudu wazuri (normal flora) ambao wapo ukeni siku zote kukulinda dhidi ya wadudu waletao magonjwa. Mazingira yao yanapokuwa sio rafiki hupelekea wao kufa na kuacha nafasi kwa wadudu waletao magonjwa.
👌👌Dalili ni kama zifuatazo😷
👉Uchafu wenye rangi ya damu ya mzee au njano ukeni
👉Kutokwa na harufu mbaya ukeni ambayo iko kama shombo la samaki.
👉Kupata muwasho au maumivu wakati wa kukojoa
👉Muwasho ukeni
👉Uke kuvimba na kuwa mwekundu
👉Kutoka damu ukeni wakati wa tendo la ndoa
Mara chache tatizo hili hupelekea kupata tatizo la maambukizi kwenye viungo vya uzazi (PID)
Pia linasababisha kuta za uke kuwa laini hivyo ni rahisi kupata mchubuko na kupata magonjwa ya zinaa.kama HIV ,
💞💞VISABABISHI VYA BACTERIA VAGINOSIS💞💞
Mazingira yao huharibiwa na vitu kama
👌Kutumia sabuni zenye kemikali ukeni
👌Kusafisha uke hadi ndani kabisa.
👌Matumizi holela ya dawa za ant biotic
👌Vitanzi vya uzazi wa mpango
👌Kuingiza vidole ukeni
✍️✍️ JINSI YA KUJIKINGA📌📌
📌Epuka kusafisha uke na bidhaa zenye kemikali tumia maji safi tu kusafisha uke
📌Tawaza kwa kutokea mbele kurudi nyuma
📌Usisafishe uke hadi ndani kabis
📌Endapo umewahi kusumbuliwa na tatizo hili basi usitumie njia ya uzazi wa mpango ya kitanzi.
📌Epuka kuingiza vidole ukeni (douching)
✍️✍️ MwanaApp.#online clinic 👩‍⚕️👩‍⚕️
www.mwanatech.com

No comments:

Post a Comment