Monday, April 27, 2020

Maneno 20 Ambayo Hutakiwi Kumwambia Mtoto wako 🤐

 Mara kadhaa wazazi wamekuwa wakiwaambia watoto wao maneno mbalimbali wakati wakiwa na furaha au hasira. Ipo nguvu kubwa kwenye maneno ya kutamkiwa ambayo wazazi wengi hawaifahamu.humjengea picha ya maisha yake ya baadae.👇👇

Kwa hakika maneno yanaweza kujenga au kubomoa maisha ya mtoto kwa kiasi kikubwa. 
🎯 fahamu maneno 20 ambayo hutakiwi kumwambia mtoto wako.

1. Wewe ni mtoto mbaya na sikutaki

👉👉Wazazi wengi wanapokasirishwa na mtoto humwambia wewe ni mtoto mbaya, hili humfanya mtoto ajione hafai.
Hii vyema kuepuka kumwambia mtoto neno hili badala yake mweleze kosa lake na athari zake ili aliepuke.

2. Kwanini usiwe kama Mwenyio HIVI humuoni???

Kauli hii humfanya mtoto ajione dhaifu kwa sababu unamlinganisha na wengine. Kauli hii pia humjengea chuki na wivu kwa wale unaowataja kwake kuwa ni bora. Hili husababisha watoto kuchukiana kwa kuwa mzazi anapenda baadhi yao au mmoja wao.haya maneno yatakuvunjia heshima Siku Moja.

3. Huwezi / unajichosha tuu.

🎯Mwache mtoto ajaribu ashindwe na si wewe kumwambia kuwa hawezi. 
*Bora kujaribu kuliko kushindwa kujaribu*
Wewe kama mzazi unapaswa kuwa hamasa kwa mtoto na si kumkatisha tamaa.

4. Usiongee na mimi/ Toa kelele zako

👉👉Ukiwa umekwazwa na mambo yako, usihamishie matatizo hayo kwa mtoto.Kumbuka mtoto naye ana haki ya kusikilizwa, msikilize na umjibu kama inavyotakiwa.Utamfanya ajihisi mnyonye na kutojiamini.

5. USIWE NA TABIA ZA KIKE WEWE.👌👌👌👌👌👌👌👌👌👌👌

💅NENO hili humwonyesha kuwa kuna jinsia fulani bora au yenye nguvu zaidi. Hivyo ni vyema kutokumwambia mtoto neno hili, mwache akue na atatambua mwenyewe kama kuna jinsia dhaifu au yenye nguvu zaidi.💪💪

6. Niache/ USINISUMBUE

Wazazi wengi hupenda kuwaambia watoto wao “niache” “nina kazi niache” “usinisumbue”, n.k. Kumbuka kuwa wewe ni kila kitu kwa mtoto wako, je unataka akuache aende kwa nani?
👈Tenga muda  uwe karibu na mtoto wako ili umuhudumie na kumsaidia kuweza kujua kipaji chake.👇👇

7. Hakuna mtu anatamani  mtoto kama wewe 

👉Wazazi huwajengea watoto roho ya kukataliwa tangu wakiwa wadogo sana. Kumwambia mtoto maneno haya humfanya ajione duni na mwenye kukataliwa; hivyo epuka maneno haya.hata akiwa mkubwa atashindwa Kuwa na ushirikiano na WENGINE 🚦

8. Umeshakuwa usifanye hivi

Jumkumu lako siyo kumhamisha mtoto hatua moja ya ukuaji kwenda hatua nyingine bali ni kumlea sawa sawa na maadili.
Kama mtoto anamalizia utoto wake mwache amalizie asije akacheza ukubwani. Mwache afurahie na kuutumia utoto wake vyema kwani kuna kipindi atacha utoto yeye mwenyewe.

9. Wewe ni mvivu/UNALOLOTE.

🎯🎯Mtoto akishatambua kuwa wewe unamwona ni mvivu, kamwe hawezi kuwa na bidii ya kazi hapo  ndo  atakuletea kero kabisa . mhamasishe na kumtia moyo badala ya kumwambia maneno mabaya.

10. Unaninyima raha wewe mtoto

💔 watoto wanapowakwaza wazazi, wazazi huwaambia kuwa wanawanyima raha. Je kama unamwambia mtoto kuwa yeye siyo chanzo cha furaha kwako ni nani atakayekupa furaha?
Mtoto akijua kuwa yeye hakupi furaha, wala yeye hatokuona kuwa wewe unamaana yeyote kwake ,hata Siku akifanikiwa kimaisha Ni ngumu Sana kukusaidia Ukiwa hujiwezi.

11. lazima ufuate sheria zangu tuu

🎯🎯Mzazi kujifanya mtemi na kabaila wa kikoroni itamfanya Mtoto awe mtumwa wa fikra na Kukosa kujiamini pale atakapokuwa mkubwa ,hii huwafanya WATOTO kuishi ndoto za wazazi wao .

12. Mali zangu zote hizi ni zako

💖Inawezekana unazo  mali nyingi ambazo kweli kabisa ni za mtoto wako, lakini unapaswa kumjengea mtoto akili ya kutafuta na si kumpumbaza kwa mali ulizo nazo.
🧠Kumwambi mtoto kila kitu changu ni chako, humfanya asifanye bidii au aone ana haki ya kupata na kutumia kila kitu jinsi apendavyo.

13. Nakupenda kuliko watoto wangu wote❤️❤️❤️❤️❤️❤️

Kauli hii humfanya mtoto awe mbaguzi na aone kuwa kuna ubaguzi na upendeleo kwenye familia. Hata kama unampenda mtoto fulani zaidi, basi usimwambie mtoto mwingine.kauli hizi kunasiku zitakukosesha Amani ndani ya familia yako.

14. Chochote unachotaka nitakupa

📈📉Kama unaijua kesho yako Basi tamka maneno hayo🌓
Kauli hii ni mbaya humfanya mtoto akutawale na aone kuwa unatakiwa kutii, kukubali na kumpa kila anachokitaka.sina maana ya kumnyima Mahitaji yake muhimu ila mfundishe Kuna Kupata na Kukosa kwenye maisha.

15. Sitaki uongee na Watu fulani.

🤔🤔Kwenye maisha Hakuna Kitu kibaya Kama kurithishwa MAADUI
Kama una chuki zako, zimalize wewe mwenyewe na si kuzihamishia kwa mtoto. Mtoto anapokuja duniani hutafuta kujenga mahusiano na watu na si kujenga chuki na matengano.

16. Sitakusamehe milele🙏🙏

🤲. Ikiwa wewe humsamehi anapokukosea, je unafikiri atakuwa na roho ya kusamehe wengine? Mfundishe mtoto kusamehe.
🤝Unapo samehe kunafaida kubwa kiafya kuliko yule aliye kukosea👇👇👇

17. Ngoja Aje Mtu fulani akupige ,mfano BABA

💪💪Hii ni kauli inayopendwa sana na wazazi wengi hasa wakina mama.Timiza wajibu wako acha kuwatengenezea chuki wengine.
Kauli hii  humfanya mtoto amwogope baba na amwone kama adui, pia humfanya mtoto amwone mama kuwa ni dhaifu, ikiwa baba hayupo mtoto atafanya makosa kwani anajua mama hamfanyi kitu anaona humuwezi. Mama Kama unatoa Kauli hizi kunasiku zitakutafuna tuu mwenyewe 👌👌

18. Matusi na kumwita majina mabaya👉👉👉

Tabia za mtoto Mara nyingi na matokeo ya matendo ya wazazi. Utamkuta mama anamwita mtoto mbwa wewe, ng’ombe, shetani, jambazi, paka, nguruwe, mbuziiii duuu bila hata aibu n.k. je kweli ulizaa vitu hivi na si binadamu?je Siku akikwambia hata wewe mbwa utajisikiaje,naomba tuwaite WATOTO Majina mazuri.
. Pia humwathiri kisaikolojia na kiroho na kumfanya awe kama kile unachomwita.

19. Nitakumaliza au nitakuua

👉👉Baadi ya wazazi huenda mbali zaidi na kuwaambia watoto wao maneno ya kuwatishia kuwadhuru vibaya au kuwaua.
Hili humwathiri mtoto kisaikolojia na kumjengea tabia ya kuwatishia au kuwadhuru watu wengine. Kama mtoto anatishiwa kuuwawa na wewe ni nani atakayemlinda?

20. Acha kulia haraka / Toa makele

🎯Kitendo Cha kulia na Kutoa machozi kina faida nyingi na kumfanya mtu aishi miaka mingi.
Kulia ni njia moja wapo ya mtoto kueleza hisia zake. Kumzuia mtoto kulia ni sawa na kumkataza kuweka wazi hisia zake. Mwache alie kama hana maradhi, kwani baada ya muda atachoka na kunyamaza mwenyewe
🎯🎯MUOMBE MUNGU AKUPE HEKIMA NA MAARIFA YA KUMLEA MTOTO .
✍️DR.CHILO.
🙏🙏MUNGU ATIMIZE HITAJI LA MOYO WAKO🙏🙏

No comments:

Post a Comment