✍️Dr.chilo.💓 online clinic⚕️
🌹🌹 Kawaida ujauzito kwa mwanamke hudumu ndani ya wiki 40 ambapo kwa jumla ni sawa na miezi tisa. Ndani ya kipindi hicho mwilii wa mwanamke hupata mabadiliko mengi,hutokana na ukuaji wa mtoto ndani ya tumbo la uzazi. Mabadiliko hayo ndani ya mwanamke mjamzito kwa kitaalamu hutokea kwa vipindi vitatu ambavyo ni;
1️⃣ Kipindi cha kwanza (first trimester)
2️⃣ Kipindi cha pili( second trimester),
3️⃣ Kipindi cha tatu( third trimester).
🤰🤰 Ni ndani ya vipindi hivi ambapo mtoto huchukua hatua ndogo ndogo za ukuaji na vipindi hivi hufahamika kulingana na wiki ambazo mwanamke mjamzito amezifikisha.
🍎🍎Ni kweli kwamba kuna haja kubwa ya wanawake wajawazito kufanya mazoezi kutokana na kwamba miili yao huitaji kuwa na nguvu na imara ili afya ya mtoto iweze kuimarika vyema.
🤰Faida ya wanawake wajawazito kufanya mazoezi ni kwamba
👍👍Ukuaji wa mtoto ndani ya mama mjamzito huleta mabadiliko katika mfumo wa mwili wa mwanamke kwa namna nyingi kama vile.
🌷🌷Uvutaji pumzi,
🌷🌷Mzunguko wa damu,
🌷🌷Mapigo ya moyo
🌷🌷Mpangilio wa misuli ndani ya mwili wake.
🌷🌷mfumo wa Hormone
🌷🌷Hadi mfumo wa tabia.
🔔🔔Mazoezi kwa wanawake wajawazito hupaswa kufanywa kwa kuzingatia vipindi vitatu vya ujauzito kama nilivyo elezea awali.
🌺🌺Ndani ya vipindi hivyo vitatu mwanamke mjamzito anapaswa kufanya mazoezi kulingana na kipindi alichopo ili aweze kupunguza uwezekano wa majeraha kutokana na mabadiliko yaliyoletwa na ujauzito pia kuepusha kuhatarisha maisha ya mtoto.
1️⃣💓Kipindi cha kwanza(first trimester)
Hutokea kwanzia pale mtoto anapotungwa tumboni mwa mama yake mpaka wiki ya 12. Ndani ya wiki hizo kumi na mbili ndipo mgongo na ubongo huanza kujitengeneza kwa mtoto tumboni na pia misuli inayotengeza umbo lake huanza kuonekana.Mwanamke mjamzito ndani ya wiki hizi kumi na mbili asiye na historia ya kufanya mazoezi anashahuriwa kufanya mazoezi ya kawaida kama vile;
🤰🤰●Yoga🌺🌺
Ambapo atanyoosha misuli ya mwili na kumfanya ajisikie vizuri na mwenye afya, zoezi hili maranyingi hufanyika kwa kukaa chini na sehemu tulivu. Japo unaweza fanya sehemu yoyote.
🤰🤰●Kutembea.🌹🌹
Ambapo kwa kutembea kutamfanya aweze kupunguza uwezekano wa mwili wake kuvimba kwa kukaa sehemu moja na pia kujenga pumzi.
🤰🤰Kucheza aerobics🍎🍎
Kwa kufanya mazoezi ya aerobics kutamwezesha kufanyisha moyo mazoezi kwa kusukuma damu kwa wingi,pia kutamsaidi kutokuvimba kwa mwili. Mazoezi haya unaweza kufanya kwenye ngazi au kitu chenye mfano wa ngazi, unakuwa unapanda na kushuka kwenye ngazi hiyo moja tu.
Kwa mwanamke mwenye uzoefu katika ulimwengu wa mazoezi anaweza akafanya mazoezi zaidi kuliko mwanamke ambaye hana historia ya kufanya mazoezi. Mazeozi ya nyongeza ukitoa yale ambayo mwanamke asiye na historia ya mazoezi anayoweza kufanya ni kama vile;
🤰🤰Squat🍎🍎
Ambapo kwa kufanya hili mwanamke mja mzito mwenye uzoezi wa mazoezi anaweza akajenga nguvu zaidi ya miguu.
Mazoezi haya hufanyika kwa kutanua miguu kiasi kasha unakuwa kama unataka kuchuchumaa lakini hufiki chini, huku mikono yako unanyoosha mbele, fanya hivyo kwa kwenda chini na juu. angalau dakika 15 tu usifanye mazoez Hadi uchoke Sanaa,hii Husaidia Miguu isivimbe na kufangazi.
🤰🤰Kuogelea🏊🏊
kwa kufanya mazoezi ya kuogelea mwanamke mjamzito anaweza kuongeza nguvu ya viungo vyake vya mwili na pia kujenga pumzi .
2️⃣Kipindi cha pili (second trimester) 🤰
🤰🤰Kipindi hiki hutokea kunzia wiki ya 13 na humalizika hadi wiki ya 27.
Ndani ya kipindi hiki ndipo mtoto anapoanza kuongezeka misuli ya mwili wake, ngozi yake huanza kuonekana na pia mwili wa mtoto hukua hadi inch 4 mpaka 5. Mwanamke mjamzito ndani ya kipindi hiki huonekana kuwa na tumbo kubwa kidogo ukilinganisha na kipi cha kwanza, na pia mazoezi anayopaswa kufanya ni machache ukilinganisha na mazoezi ya kipindi cha kwanza.
Mazoezi anayoweza kuafanya mwanamke mjamzito ndani ya kipi hiki ni;
📌📌Mazoezi ya kujinyoosha.
Kwa kufanya mazoezi ya kujinyoosha(stretching) kunaweza kuweka mwili wake katika hali nzuri ambapo hatopata maumivu ya viungo kama vile mgongo na mengineyo.
🤰🤰●Kutembea💃💃
Kwa kufanya mazoezi haya ya kutembea kunaweza kumsaidia mjamzito kutokuvimba kwa miguu yake na pia kusaidia kwenye suala la pumzi.
🌺🌺●Yoga
Kutokana na ukubwa wa tumbo kwa kipindi hiki na kushindwa kufanya mazoezi mengi kwa mama mjamzito basi ni vyema kufanya zoezi hili ili aweze kujinyoosha na kutengeneza afya ikawa poa.
3️⃣Kipindi cha tatu(third trimester) 🤰🤰
kipindi hiki huanzia kutoka wiki ya 28 na humalizikia wiki ya kujifungua. Ndani ya kipindi hiki ndipo mwanamke mjamzito hula sana kutokana na kwamba umalizikiaji wa ukuaji wa mtoto tumboni hutokea.
🍎🍎Kipindi hiki ndipo mwanamke mjamzito anapaswa kuwa mwangalifu ambapo atapaswa kupunguza kazi nyingi na mazoezi mazito, na hivyo anapswa kufanya mazoezi marahisi.
Mazoezi ambayo anayoweza kufanya mwanamke mjamzito kwa kipindi hiki ni;
●Kutembea💃💃
Mwanamke mjamzito ndani ya kipindi hiki hushauriwa sana kufanya mazoezi ya kutembea kwa umbali mdogo ili aweze kupunguza uwezekano wa kuvimba miguu yake na pia humsaidia kwenye suala la pumzi.
●Mazoezi ya kujinyoosha
Kwa kufanya mazoezi ya kujinyoosha(stretching) kwa mwanamke mjamzito wa kipindi hiki cha mwisho kunaweza kumsaidia mwili wake kwa kuuweka katika hali nzuri ambapo hatopata maumivu ya viungo kama vile mgongo na mengineyo.
🤰🤰HITIMISHO 📌📌
FANYA mazoezi kwa kiasi ,na jiepushe na kunywa pombe , Uvutaji wa sigara na migogo isiokuwa ya lazi na watu wako wa karibu ,
🤰🤰 Dr.chilo .💓NINA WAPENDA SANA.MUNGU ATIMIZE HITAJI LA MOYO WAKO.
📌📌TOA MAONI HAPO CHINI.
No comments:
Post a Comment