❣️Nini Kinasababisha Kukosa Hedhi?❣️❣️
✍️ Dr CHILO 💞 online clinic 💡
Amenorrhea inaweza kutokea kwa sababu nyingi. Baadhi zikiwa ni za kawaida katika maisha ya mwanamke, wakati nyingine zikisababishwa na matumizi ya madawa au zikiwa ni ishara ya tatizo la kiafya. Tatizo la kukosa hedhi linaweza kusababishwa na dosari yo yote kwenye hypothalamus, pituitary, ovari, mkondo wa uke au ya kiutendaji kimwili.
Sababu za kawaida
. Ujauzito
. Kunyonyesha
. Kukoma hedhi
Dawa za Kuzuia Mimba
Wanawake wengine wakitumia vidonge vya kuzuia mimba hukosa hedhi. Hata baada ya kuacha matumizi ya vidonge hivyo, huwachukua muda miili yao kurudi kwenye hali za kawaida na kuanza kuona hedhi zao. Njia za sindano au kupandikiza zaweza pia kuleta tatizo la kukosa hedhi.
❤️❤️Mitindo Ya Maisha
Baadhi ya mitindo ya maisha huweza kuchangia mwanamke kukosa hedhi. Kwa mfano:
. ✍️Kuwa na uzito mdogo sana. Kuwa na uzito mdogo kupita kiasi – asilimia 10 chini ya uzito wa kawaida – husimamisha shughuli nyingi za homoni ndani ya mwili, hivyo kusimamisha uzalishaji wa mayai
✍️. Mazoezi zaidi ya kawaida. Wanawake wanaoshiriki shughuli zinazodai mazoezi ya juu, hujikuta wakipoteza hedhi zao. Baadhi ya sababu zinachangia kwa wanariadha, ikiwa ni pamoja na uzito mdogo, kuwa na mafuta kidogo ndani ya mwili, msongo wa mawazo na matumizi makubwa ya nishati ya mwili.
.✍️ Msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo huweza kubadilisha kwa muda utendaji kazi wa hypothalamus – sehemu ya ubongo inayosimamia homoni zinazoratibu hedhi. Uzalishaji wa mayai na hedhi, hivyo vyaweza kusimama. Hedhi za kawaida hurudi baada ya msomgo wa mawazo kupungua.
✍️Kukosa Uwiano Wa Homoni
Matatizo kadhaa katika viungo vya mwili huweza kuvuruga mpangilio wa homoni katika mwili,
♥️♥️♥️ MwanaApp⚕️⚕️⚕️
No comments:
Post a Comment