Saturday, April 11, 2020

JE UKIJIFUNGUA LINI UANZE KUFANYA TENDO LA NDOA?JIBU HILI HAPA

💞💞 hili swali wanawake wengi hujiuliza baada ya kujifungua, lini nianze kumpa Utamu???? lakini kitaalamu ni kwamba uwe umezaa kwa upasuaji au kwa njia ya kawaida hutakiwi kushiriki tendo la ndoa mpaka wiki sita ziishe na wiki sita sikishaisha wewe mwanamke unaweza kujitafakari kama uko tayari au bado kwa ajili ya tendo hilo yaani kwa sababu za kisaikolojia zaidi yaani uchovu na msongo wa mawazo.

je kwanini sio vizuri kushiriki tendo la ndoa kabla ya wiki ya sita?

💞maumivu kipindi cha tendo la ndoa;
 hii husababishwa na mabadiliko makubwa ya viwango vya homoni mwilini hasa kupanda kwa homoni ya kutoa maziwa ya mama kitaalamu kama prolactin na kushuka kwa homoni za uzazi yaani progesterone na eostrogen, hii inaweza kusababisha uke kuwa mkavu sana na kuleta maumivu wakati wa tendo.
nini cha kufanya? muuleze kistaarabu mpenzi wako kuhusu hili na aelewe kwamba ukavu wako hausababishwi na kupungua kwa mapenzi yako kwake, lakini hata baada ya wiki ya sita ukavu huu unaweza kuendelea hivyo mnaweza kutumia vilainishi kama ky gel kusaidia hili.
🌹ladha ya tendo la ndoa haitakua kama mwanzo;🌺🌺
hii ni sababu ya kupanuka sana kwa misuli ya uke hivyo mwanamke anakua hausikii vizuri uume kama mwanzo na unaweza kuona kama hakuna ladha tena.
nini cha kufanya?
fanya mazoezi ya kegel, mazoezi haya yaligunduliwa na doctor arnord kegel mwaka 1948 ambaye alikua bingwa wa magonjwa ya kina mama yaani obstretic and gynacology specialist..mazoezi haya hufanywa kwa kubana msuli ambao unautumia kuzuia mkojo wakati wa kukojoa, sasa bana msuli huu wakati hauna mkojo kwa sekunde kumi na kuachia kwa sekunde kumi...fanya mara tatu asubuhi mchana na jioni na uke wako utarudi kua mdogo kama zamani.

💞matiti baada yanatoa maziwa mengi;

 hii inaweza ikafanya tendo la ndoa lisiwe la furaha sana hasa wakati mwanamke anafika kileleni maziwa yanaweza kumwagika mengi sana na hii pia inaweza kuendelea mpaka zaidi ya wiki ya sita sababu mtoto anakua bado anaendelea kunyonya na hata usipompa titi maziwa yataendelea kutoka.
nini cha kufanya? jitahidi kuvaa sidiria nzito wakati wa tendo la ndoa kuzuia hali hii ambayo inaweza isiwe nzuri hasa kwa mwenzi wako.

🌹🌹huna amani na mwili wako; 💝💝
huchukua mpaka miezi miwili kwa tumbo la uzazi kurudi kwenye hali yake ya zamani. yaani mtu akizaa anakua bado anamuonekano wa mtu mwenye ujauzito wa miezi sita, na kurudi kwenye uzito wa zamani inaweza kuchukua mpaka mwaka mmoja kama ukifanya mazoezi na usipofanya unaweza kubaki vilevile au kuongezeka.[watanzania wengi hawafanyi mazozi baada ya kuzaa na hunenepa zaidi]
nini cha kufanya?
usiwe na wasiwasi sana kwani mume wako anaelewa mabadiliko ya mwili wako yanasababishwa na uzazi, lakini pia penda ulichokipata kwani mpaka umepata huyo mtoto umepitia mateso makubwa ya jasho na damu. kikubwa anza mazoezi pale utakapokua tayari.

💝💝kuna hatari ya kubeba mimba nyingine ?;

 Ndio ,japokua uwezekano wa kubeba mimba nyingine baada ya kujifungua hua ni mdogo sana lakini sio kwamba haiwezekani kabisa kwani mimi binafsi nimekutana na watu waliobeba mimba kipindi hiki. hii ni sababu ya kuchelewa kuanza kuona siku zako za hedhi na kutoona siku zako kunaweza kukufanya ushindwe kuhesabu siku zako za  hatari.

💞vidonda bado havijapona;💞
 kama ulizaa kwa upasuaji au njia ya kawaida bado kuna vidonda ndani ya uke na uzazi ambavyo vilisababishwa na mtoto kupita ukiachilia mbali kidonda cha upasuaji ambacho mara nyingi hua hakina hali nzuri kabla ya wiki ya 6. hivyo ukishiriki tendo la ndoa unaweza kusababisha magonjwa yaani infection na kuugua, kusabaisha kuachia kwa mshono wa upasuaji au kuhatarisha afya ya kizazi kwa ajili ya watoto wajao.
nini cha kufanya?
mueleweshe mume wako kuhusu uwezekano wa kupata magonjwa na atakuelewa.

🌹🌹mwisho;🌹🌹
hali hii ni ya muda tu, wewe kama mwanamke kua mstari wa mbele kuhakikisha unapona mapema na kurudi katika hali yako ya zamani, ndoa nyingi huanza kuharibika hapa kwani wanawake hutumia nafasi hii kuwanyima unyumba waume zao kwa muda mrefu sana kwa kisingizio cha uzazi huku wakisahau kwamba huko nje kuna wakware wanasubiri ushindwe huku ndani wambebe mumeo.

🌺🌺 ASAAAAAAANTEEE 💞💞
KURUDI KWENYE UBORA BAADA YA KUZAA INAWEZEKANA ?💖💖
toa maoni yako hapo chini.

No comments:

Post a Comment