Sunday, April 12, 2020

DALILI ZA UJAUZITO

✍️Dr.chilo🌹 online clinic⚕️
👩‍⚕️👩‍⚕️🤰Dalili za ujauzito hutofautiana kati ya mwanamke mmoja  na mwanamke mwingine, ingawa kuchelewa au kukosa hedhi ni dalili moja muhimu sana ya ujauzito Lakini Kumbuka Kukosa hedhi kunaweza sababisha na vitu vingi Sio Mimba tuu..

🌺🌺Ni muhimu kuzitambua na kuzifahamu dalili hizi kwa sababu zinaweza kusaidia kujua kama kweli umeshika ujauzito au la  pamoja na kuweza kutofautisha matatizo mengine yanayoshahabiana kwa dalili na  ujauzito.

Hebu sasa tuangalie dalili na ishara za ujauzito:

🤰Kutokwa damu kidogo ukeni wakati kiumbe kikipandikizwa kwenye mfuko wa uzazi, ingawa siyo wanawake wote hupatwa na dalili hii🌺🌺

🤰Kukosa hedhi, hii ni moja ya dalili kubwa ya ujauzito🌺🌺

🤰Maumivu kwenye matiti na kuvimba matiti (huweza kutokea kati ya wiki ya 1 hadi ya 2)🌺🌺

🤰Uchovu, wanawake wengi huhisi uchovu na  na hali ya kutopenda kufanya lolote.🌺🌺

🤰Kupoteza ladha au kuhisi ladha ya chuma mdomoni🌺🌺

🤰Kuongezeka kwa hisia ya harufu, kipindi cha ujauzito wanawake wengi huongezeka hisia ya harufu🌺🌺

🤰Kichefuchefu na kutapika🌺🌺

🤰Maumivu ya kichwa🌺🌺

🤰Kizunguzungu🌺🌺

🤰Kukojoa mara kwa mara (hasa kati ya wiki 6-8)🌺🌺

🤰Kubadilika rangi kwa ngozi inayozunguka chuchu kuwa nyeusi🌺

🤰Kutamani baadhi ya vyakula na kuchukia vingine🌺🌺

🤰Tumbo kujaa au kuvimbiwa🌺🌺

🤰Kununa na kukasirika haraka au kuanza kuchukia / kuwapenda zaidi baadhi ya watu.🌺🌺

🤰Kiungulia au kupata choo kigumu🌺

🤰Kolostramu kuanza kutoka kwenye matiti 🌺🌺

🤰Kuongezeka uzito🌺🌺

🤰Kuweza kupapasa mtoto (palpation of the baby)🌺🌺

🤰Kulainika na kuvimba kwa shingo ya uzazi (Hegars sign) - kuanzia wiki ya 6

🤰Shingo ya uzazi kubadilika rangi kuwa ya samawati kutokana na msongamano wa damu katika mishipa ya vena. Ishara hii hujulikana kama Chadwick's sign🌺


Dalili nyingine ni pamoja na

🌺Mstari wima mweusi hutokea tumboni kuanzia chini ya kitovu (linea nigra)💖💖

🌺Mama kuhisi mtoto akicheza (kuanzia wiki ya 20)💖💖

🌺Maumivu ya mgongo hasa mimba ikishakuwa kubwa.💖💖

🌺Kipimo cha mimba kuwa chanya (positive).💖💖

🌺Kusikia mapigo ya moyo ya mtoto💖

🌺Mtoto kuonekana kwenye kipimo cha ultrasound💖💖

💞💞KUMBUKA kupika kituo Cha Afya mapema pale unapohosi unaujauzito.
✍️✍️ ASAAAAAAANTEEE.
TOA MAONI HAPO CHINI

No comments:

Post a Comment