Saturday, April 4, 2020
♂️JINSI YA KUPANGA KUPATA MTOTO WAKIUME/WAKIKE.♀️
✍️Dr.chilo👩⚕️ MwanaApp
Tambua ili urutubishwaji(fertilization) ufanyike ni lazima mbegu ya kiume (manii) ikutane na mbegu ya kike (ova).
Mbegu ya kiume huwa tayari muda wowote kurutubisha yai la kike lililopevuka mara moja kwa kila mzunguko(mwezi).
Yai la mwanamke huwa na chromosome XX wakati mbegu ya kiume huwa na XY.
Ifahamike kuwa wakati wa kujamiiana mwanaume hutoa mbegu zilizobeba chromosomes zote mbili (X Y)kwa pamoja, itakayowahi kurutubosha yai la kike ndio itaamua jinsia ya mtoto. kwa maneno mengine ni kwamba jinsia ya mtoto atakayezaliwa inategemea zaidi chromosome gani ya baba itakayokutana na yai la kike. "chromosome ya mwanaume ndio huamua jinsia ya mtoto"
mfano
1. yai lakike (X) Likakutana na chromosome 👍 kutoka kwa mwanaume = Mtoto wa kiume atazaliwa (XY)
2. yai lakike (X) likakutana na chromosome (X) kutoka kwa mwanaume =mtoto wa kike atazaliwa (XX).
Sifa za chromosome Y
1. Inatembea kwa kasi kubwa zaidi ndani ya mfumo wa uzazi wa mwanamke, kama yai la kike lipo tayari yenyewe itawahi kurutubisha
2. Zina maisha mafupi(life span) kulinga isha na X , zikitolewa huweza kustahimili kwa muda kati ya masaa 24-48.
3. Ni dhaifu kwenye acid (tindikali) ya uke ikikaa kwa muda mrefu
Sifa za chromosome X
1. Ina kasi ndogo kulinganisha na Y
2. Inaduma kwa maisha marefu kuliko Y mpaka masaa 72 baada ya kutolewa,hivyo huvumilia kwa muda mrefu hatakama bado yai lakike halijatoka
3. Inastahimili acid (tindikali) ya uke kwa muda mrefu
Mambo ya kuzingatia
1. Uwepo ushirikiano wa kutosha kati ya wenzi
2. Mwanamke ajue mzunguko wake na usiwe wenye kubadilika mara kwa mara
3. Ph ya uke iwe 4-5.5 (normal)
4. Mwanamke ajue siku zake hatari ambazo yai linakuwa tayari kwa kurutubishwa, unaweza kujua kwa kuangalia ute unaotoka unakuwa mweupe(transparent) na mzito kama wa kwenye yai lakuku
1. Kupata mtoto wa Kiume
👉🏽 kujamiiana siku ambayo yai la mwanamke linatoka iwe rahisi chromosome Y kukutana na X, kwa wasiofahamu siku ya yai kutoka wanaweza kutumia njia ya kuangalia ute wa siku za hatari ndio kiashiria cha kuonesha yai limeshatoka(ovulation)
👉🏽kushiriki tendo siku ya 13-15 kwanzia hedhi ilipoanza
👉🏽Usifanye tendo siku 2 kabla au baada yayai kushuka
👉🏽Style ya kujamiiana inayoruhusu uume kuingia ndani zaidi ili kufanye mbegu zifike haraka
👉🏽Mwanamke afike kileleni kabla ya mwanaume, anapofika kileleni anatoa maji yenye asili ya alkali ambayo ni mazingira rafiki kwa chromosome Y yenye kuleta mtoto wa kiume
👉🏽Mwanamke atumie vyakula vya chumvuchumvi, potassium na sodium kwa wingi ili kuongeza hali ya alkaline ukeni
2. Mtoto wa kike
👉🏽tendo la ndoa lifanyike siku 3 kabla au siku 3 baada ya yai la kike kutolewa(ovulation) au kabla ya kuona ute hii itasaidia chromosome Y ishindwe kuishi kwa muda hadi yai latakapotoka lataikuta X pekee na kutengeneza mtoto wa kike
👉🏽tendo lifanyike siku ya 10-13 kabla baada ya hedhi kuanza, na kwanzia siku ya 16 nakuendelea
👉🏽style ya tendo isiwe ya kusababisha uume kuzama ndani sana ili kuzuia Y kufika mapema
👉🏽tendo la ndoa lifanywe kabla au baada ya ovulation (yai la kike kutolewa)
👉🏽Mwanamke ale vyakula vya acid kwa wingi ili kutengeneza hali ya alkali ukeni inayosaidia chromosome X kuishi muda mwingi
♂️Mwisho.🌺
Njia hizi zinauhakika wa hadi 75% na asilimia zaidi kama tendo la ndoa litafanywa siku 3 kabla ya siku za hatari (kunasa ujauzito), lakini kumbuka
”njia za Mungu ni bora zaidi ya wanadamu"
Mungu ndiye huamua jambo lolote atakalo na likawa
"mweleze hitaji lako akutimizie"
💓💓MUNGU awatangulie mama vijacho Wote.
🤰🤰Toa comments hapo chini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment