Saturday, May 23, 2020

FAIDA ZA KUFANYA MAPENZI NA LINI UACHE KUFANYA UKIWA NA MIMBA

 
FAIDA  ZA KUFANYA MAPENZI KIPINDI CHA UJAUZITO 🍎
✍️✍️DR.CHILO

🤰💞Kuna watu wamekua wakiuliza mara kwa mara kama inaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa mpaka umri gani wa mimba au ni sahihi kufanya tendo la ndoa kipindi cha ujauzito?

✍️Mwanamke akiwa na mimba anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa hata kama anatarajia kuzaa kesho yake, hakuna tatizo lolote linalomzuia kufanya hivyo, baadhi ya wanawake wamekua wazito sana kufanya hivyo kwa kua na sababu mbalimbali za kujitetea bila kujua kwamba wanazikosa faida hizi ambazo ni muhumu kiafya.faida zenyewe ni kama zifuatazo:

1️⃣Husaidia uchungu mzuri na kupona mapema; kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa huambatana na kubana kwa misuli ya nyonga hii husaidia kuweka imara misuli ya nyonga ambayo ni muhimu sana wakati wa kusukuma mtoto na baada ya kuzaa kwani misuli hii ikiwa legevu mwanamke huweza kushindwa kuzaa kwa njia ya kawaida na hata baada ya kuzaa huweza kushindwa kuzuia mkojo usitoke wenyewe au kuvuja damu kwa muda mrefu.
2️⃣Hupunguza kwenda ovyo kukojoa au kujikojolea; wakati wa ujauzito mtoto anapozidi kua mkubwa anazidi kukandamiza kibovu cha mkojo, hii humfanya mama aende chooni kukojoa mara kwa mara na wakati mwingine hata akipiga chafya au kukohoa basi mkojo unaweza kutoka wenyewe. tendo la ndoa huibana misuli ya nyonga na kuzuia hali hii.
3️⃣Huzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba; tafiti zinaonyesha kwamba aina ya protini inayopatikana kwenye mbegu za mwanaume huongeza kinga ya mwili na kuzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba ambacho kinaua wanawake wengi sana.

4️⃣Hutibu tatizo la kufika kileleni kwa shida; kipindi cha ujauzito chuchu za mwanamke na kinembe chake huvimba na kuongezeka hisia mara dufu huku kiwango cha homoni za oestrogen kikiwa juu sana, hii humfanya kufika kileleni kirahisi sana kuliko mwanzoni.5️⃣Huwapa uwezo wa kujiamini; kipindi cha ujauzito mwanamke hua anapata hofu sana na kutojiamini na mwili wake, hua na wasiwasi kwamba mwili wake unaharibika hivyo kitendo cha mwanaume wake kuendelea kushiriki naye tendo la ndoa humpa kujiamini kwamba mwili wake bado uko kwenye hali nzuri na anapendwa.kipindi Cha UJAUZITO MWANAMKE anakuwa mtamu ZAIDI.

6️⃣Hupunguza msongo wa mawazo; kipindi cha ujauzito wanawake wengi huwaza sana kuhusu kesho yao...je swala la uchumi litakuaje? mwili wangu utakuaje? je nitapata jinsia nayotegemea? na kadhalika.. tendo la ndoa hutoa homoni ya upendo kwa jina la oxytocin(hormone of love), homoni hii hupunguza mawazo na kumpa amani mjamzito.

7️⃣Huongeza upendo na mshikamano kati ya wapenzi; katika hali ya kawaida wanandoa wakikwazana wanaweza wakapatana kwa kushiriki tendo la ndoa tu, amani na upendo kipindi hiki ni muhimu sana kwani kuna mtoto anakuja ambaye anatakiwa kuzaliwa huku baba na mama wakiwa wanapatana na kupendana.

8️⃣Hukuandaa na uchungu; ukishiriki  TENDO LA ndoa wakati wa tarehe zilizokadiriwa zimefika unapata homoni moja kutoka kwenye mbegu za mwanaume kwa jina la prostglandin, homoni hii huivisha mlango wa uzazi na kuanza kufunguka taratibu kujiandaa na uchungu.

9️⃣Hutibu tatizo la kukosa usingizi; wanawake wengi wajawazito hua na dalili mbalimbali za maumivu na kuumwa sehemu tofauti za mwili na msongo wa mawazo, hii huweza kuwakosesha usingizi kabisa..tendo la ndoa huweza kuwapa usingizi mzuri Sana pale watakapofikishwa kileleni.

🔟Hupunguza presha ya damu; kipindi cha tendo la ndoa presha ya damu hushuka kwenye kiwango kizuri sana, hii ni muhimu sana kwa wanawake wenye hatari ya kupata kifafa cha mimba kama wanene sana, wenye kisukari au wenye historia za ugonjwa wa presha kwenye koo zao.

🌹🍎Hakikisha unatumia staili za tendo la ndoa ambazo hazimuumizi mtoto na mama yaani hakikisha halalii tumbo hasa mimba ikiwa kubwa,
🛌👌 kuna staili muhimu kipindi hiki kama kuangalia upande mmoja, mwanamke kuja juu, au mwanamke kuinama
🍎✍️ online clinic⚕️ MwanaApp ♥️

Monday, April 27, 2020

Maneno 20 Ambayo Hutakiwi Kumwambia Mtoto wako 🤐

 Mara kadhaa wazazi wamekuwa wakiwaambia watoto wao maneno mbalimbali wakati wakiwa na furaha au hasira. Ipo nguvu kubwa kwenye maneno ya kutamkiwa ambayo wazazi wengi hawaifahamu.humjengea picha ya maisha yake ya baadae.👇👇

Kwa hakika maneno yanaweza kujenga au kubomoa maisha ya mtoto kwa kiasi kikubwa. 
🎯 fahamu maneno 20 ambayo hutakiwi kumwambia mtoto wako.

1. Wewe ni mtoto mbaya na sikutaki

👉👉Wazazi wengi wanapokasirishwa na mtoto humwambia wewe ni mtoto mbaya, hili humfanya mtoto ajione hafai.
Hii vyema kuepuka kumwambia mtoto neno hili badala yake mweleze kosa lake na athari zake ili aliepuke.

2. Kwanini usiwe kama Mwenyio HIVI humuoni???

Kauli hii humfanya mtoto ajione dhaifu kwa sababu unamlinganisha na wengine. Kauli hii pia humjengea chuki na wivu kwa wale unaowataja kwake kuwa ni bora. Hili husababisha watoto kuchukiana kwa kuwa mzazi anapenda baadhi yao au mmoja wao.haya maneno yatakuvunjia heshima Siku Moja.

3. Huwezi / unajichosha tuu.

🎯Mwache mtoto ajaribu ashindwe na si wewe kumwambia kuwa hawezi. 
*Bora kujaribu kuliko kushindwa kujaribu*
Wewe kama mzazi unapaswa kuwa hamasa kwa mtoto na si kumkatisha tamaa.

4. Usiongee na mimi/ Toa kelele zako

👉👉Ukiwa umekwazwa na mambo yako, usihamishie matatizo hayo kwa mtoto.Kumbuka mtoto naye ana haki ya kusikilizwa, msikilize na umjibu kama inavyotakiwa.Utamfanya ajihisi mnyonye na kutojiamini.

5. USIWE NA TABIA ZA KIKE WEWE.👌👌👌👌👌👌👌👌👌👌👌

💅NENO hili humwonyesha kuwa kuna jinsia fulani bora au yenye nguvu zaidi. Hivyo ni vyema kutokumwambia mtoto neno hili, mwache akue na atatambua mwenyewe kama kuna jinsia dhaifu au yenye nguvu zaidi.💪💪

6. Niache/ USINISUMBUE

Wazazi wengi hupenda kuwaambia watoto wao “niache” “nina kazi niache” “usinisumbue”, n.k. Kumbuka kuwa wewe ni kila kitu kwa mtoto wako, je unataka akuache aende kwa nani?
👈Tenga muda  uwe karibu na mtoto wako ili umuhudumie na kumsaidia kuweza kujua kipaji chake.👇👇

7. Hakuna mtu anatamani  mtoto kama wewe 

👉Wazazi huwajengea watoto roho ya kukataliwa tangu wakiwa wadogo sana. Kumwambia mtoto maneno haya humfanya ajione duni na mwenye kukataliwa; hivyo epuka maneno haya.hata akiwa mkubwa atashindwa Kuwa na ushirikiano na WENGINE 🚦

8. Umeshakuwa usifanye hivi

Jumkumu lako siyo kumhamisha mtoto hatua moja ya ukuaji kwenda hatua nyingine bali ni kumlea sawa sawa na maadili.
Kama mtoto anamalizia utoto wake mwache amalizie asije akacheza ukubwani. Mwache afurahie na kuutumia utoto wake vyema kwani kuna kipindi atacha utoto yeye mwenyewe.

9. Wewe ni mvivu/UNALOLOTE.

🎯🎯Mtoto akishatambua kuwa wewe unamwona ni mvivu, kamwe hawezi kuwa na bidii ya kazi hapo  ndo  atakuletea kero kabisa . mhamasishe na kumtia moyo badala ya kumwambia maneno mabaya.

10. Unaninyima raha wewe mtoto

💔 watoto wanapowakwaza wazazi, wazazi huwaambia kuwa wanawanyima raha. Je kama unamwambia mtoto kuwa yeye siyo chanzo cha furaha kwako ni nani atakayekupa furaha?
Mtoto akijua kuwa yeye hakupi furaha, wala yeye hatokuona kuwa wewe unamaana yeyote kwake ,hata Siku akifanikiwa kimaisha Ni ngumu Sana kukusaidia Ukiwa hujiwezi.

11. lazima ufuate sheria zangu tuu

🎯🎯Mzazi kujifanya mtemi na kabaila wa kikoroni itamfanya Mtoto awe mtumwa wa fikra na Kukosa kujiamini pale atakapokuwa mkubwa ,hii huwafanya WATOTO kuishi ndoto za wazazi wao .

12. Mali zangu zote hizi ni zako

💖Inawezekana unazo  mali nyingi ambazo kweli kabisa ni za mtoto wako, lakini unapaswa kumjengea mtoto akili ya kutafuta na si kumpumbaza kwa mali ulizo nazo.
🧠Kumwambi mtoto kila kitu changu ni chako, humfanya asifanye bidii au aone ana haki ya kupata na kutumia kila kitu jinsi apendavyo.

13. Nakupenda kuliko watoto wangu wote❤️❤️❤️❤️❤️❤️

Kauli hii humfanya mtoto awe mbaguzi na aone kuwa kuna ubaguzi na upendeleo kwenye familia. Hata kama unampenda mtoto fulani zaidi, basi usimwambie mtoto mwingine.kauli hizi kunasiku zitakukosesha Amani ndani ya familia yako.

14. Chochote unachotaka nitakupa

📈📉Kama unaijua kesho yako Basi tamka maneno hayo🌓
Kauli hii ni mbaya humfanya mtoto akutawale na aone kuwa unatakiwa kutii, kukubali na kumpa kila anachokitaka.sina maana ya kumnyima Mahitaji yake muhimu ila mfundishe Kuna Kupata na Kukosa kwenye maisha.

15. Sitaki uongee na Watu fulani.

🤔🤔Kwenye maisha Hakuna Kitu kibaya Kama kurithishwa MAADUI
Kama una chuki zako, zimalize wewe mwenyewe na si kuzihamishia kwa mtoto. Mtoto anapokuja duniani hutafuta kujenga mahusiano na watu na si kujenga chuki na matengano.

16. Sitakusamehe milele🙏🙏

🤲. Ikiwa wewe humsamehi anapokukosea, je unafikiri atakuwa na roho ya kusamehe wengine? Mfundishe mtoto kusamehe.
🤝Unapo samehe kunafaida kubwa kiafya kuliko yule aliye kukosea👇👇👇

17. Ngoja Aje Mtu fulani akupige ,mfano BABA

💪💪Hii ni kauli inayopendwa sana na wazazi wengi hasa wakina mama.Timiza wajibu wako acha kuwatengenezea chuki wengine.
Kauli hii  humfanya mtoto amwogope baba na amwone kama adui, pia humfanya mtoto amwone mama kuwa ni dhaifu, ikiwa baba hayupo mtoto atafanya makosa kwani anajua mama hamfanyi kitu anaona humuwezi. Mama Kama unatoa Kauli hizi kunasiku zitakutafuna tuu mwenyewe 👌👌

18. Matusi na kumwita majina mabaya👉👉👉

Tabia za mtoto Mara nyingi na matokeo ya matendo ya wazazi. Utamkuta mama anamwita mtoto mbwa wewe, ng’ombe, shetani, jambazi, paka, nguruwe, mbuziiii duuu bila hata aibu n.k. je kweli ulizaa vitu hivi na si binadamu?je Siku akikwambia hata wewe mbwa utajisikiaje,naomba tuwaite WATOTO Majina mazuri.
. Pia humwathiri kisaikolojia na kiroho na kumfanya awe kama kile unachomwita.

19. Nitakumaliza au nitakuua

👉👉Baadi ya wazazi huenda mbali zaidi na kuwaambia watoto wao maneno ya kuwatishia kuwadhuru vibaya au kuwaua.
Hili humwathiri mtoto kisaikolojia na kumjengea tabia ya kuwatishia au kuwadhuru watu wengine. Kama mtoto anatishiwa kuuwawa na wewe ni nani atakayemlinda?

20. Acha kulia haraka / Toa makele

🎯Kitendo Cha kulia na Kutoa machozi kina faida nyingi na kumfanya mtu aishi miaka mingi.
Kulia ni njia moja wapo ya mtoto kueleza hisia zake. Kumzuia mtoto kulia ni sawa na kumkataza kuweka wazi hisia zake. Mwache alie kama hana maradhi, kwani baada ya muda atachoka na kunyamaza mwenyewe
🎯🎯MUOMBE MUNGU AKUPE HEKIMA NA MAARIFA YA KUMLEA MTOTO .
✍️DR.CHILO.
🙏🙏MUNGU ATIMIZE HITAJI LA MOYO WAKO🙏🙏

Friday, April 24, 2020

EPUKA VYAKULA AINA HII ILI UZAE MTOTO MWENYE AFYA NJEMA

FAHAMU VYAKULA VINAVYOFAA NA VILE VINAVYOZUILIWA WAKATI WA UJAUZITO

🍓🍓Ni vyakula gani vya kuepuka kutumiwa na wajawazito?Ili mtoto azaliwe akiwa na afya njema pamoja na akili timamu, akiwa tumboni lazima alishwe lishe bora na mlo sahihi. Mwenye jukumu la kutoa lishe bora na sahihi kwa kiumbe kilichomo tumboni ni mama. Anatakiwa kujua aina ya vyakula anavyopaswa kula. Vivyo hivyo, anatakiwa kujua aina ya vyakula vya kuviepuka.
Katika makala ya leo, tunaangalia orodha ya vyakula vilivyokatazwa. Mama mja mzito haruhusiwi kuvila vyakula vifuatavyo kwa faida ya kiumbe kilichomo tumboni na kwa faida yake mwenyewe:

💝💝Nyama mbichi💗💗

Epuka kula samaki au nyama mbichi au iliyopikwa lakini haikuiva vizuri. Utajiepusha na uwezekano wa kula bakteria na vijidudu vingine hatari kwa afya ya mtoto tumboni. Mjamzito anapokula nyama, anatakiwa kuhakikisha imeiva sawasawa.
‘Soseji” na “Sandwich”
Mjamzito haruhusiwi kula ‘soseji’, ‘sandwichi’ za nyama na vyakula vingine vilivyotengenezwa kwa nyama. Inaaminika kuwa nyama zinazoandaliwa kwa ajili ya kutengenezea vyakula kama hivyo, huwa vimewekewa vihifadhi vyakula (preservatives) ambavyo vinaweza visiwe vizuri kwa afya ya mtoto.

💝Samaki wenye zebaki (Mercury)💝

Wajawazito wamekatazwa kula samaki wenye kiasi kingi cha madini ya zebaki. Ulaji wa zebaji kwa wajawazito umehusishwa na uzaaji wa watoto taahira. Mfano wa samaki hao ni pamoja na Papa, Chuchunge na dagaa wakubwa.

💝💝Mayai Mabichi🍓🍓

Ulaji wa mayai mabichi au vyakula vilivyochanganywa na mayai mabichi, mjamzito haruhusiwi kuvila. Kuna baadhi ya ‘Ice Cream’ na ‘mayonaizi’ hutengenezwa kwa kuchanganywa na mayai mabichi. Mjamzito amekatazwa kuvila vyakula hivyo.

💝💝Maziwa mabichi🍓🍓
Maziwa mabichi huweza kuwa na bakteria ajulikanae kama ‘Listeria’, ambaye huweza kusababisha kuharibika kwa mimba. Unapokunywa maziwa, hakikisha yamechemshwa au kama ni ya paketi hakikisha ni yale yaliyoandikwa‘Pasteurized’ na siyo ‘Unpasteurized’.

💝💝Kafeini (Caffeine)🍓🍓

Ingawa baadhi ya utafiti unaonesha kuwa unywaji wa kiasi kidogo cha kafeini hauna madhara, lakini kuna utafiti mwingine unaonesha kuwa unywaji wa kafeini una uhusiano na kuharibika kwa mimba. Kafeini ni aina ya kirutubisho kinachopatikana ndani ya kahawa.
✍️✍️Iwapo mjamzito atakunywa kahawa, basi anywe kiasi kidogo sana kisichozidi kikombe kimoja kwa siku. Kwa kawaida kahawa hukausha maji mwilini, hivyo unywaji wake husaidia kukauka maji mwilini ambayo ni muhimu sana kwa mjamzito.
🎯🎯Utafiti mwingine unaonesha kuwa kafeini inahusishwa pia na uharibikaji wa mimba, uzaaji wa watoto ‘njiti’ na watoto wenye uzito mdogo. Ni vizuri kunywa maji ya kutosha, maziwa na juisi na kuepuka kunywa vinywaji vyenye kahawa.

🍓🍓🍓Pombe🍏🍏🍏

Hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa unywaji wa pombe kiasi kidogo wakati wa ujauzito hauna madhara, kwa maana hiyo matumizi ya pombe hayaruhusiwi kabisa wakati wa ujauzito, hata kama ni kidogo.
🎯🎯Unywaji wa pombe wakati wa ujauzito huweza kuathiri ukuaji mzuri wa mtoto. Kutegemeana na kiasi atakachokunywa mjamzito, pombe inaweza kumsababishia mtoto ugonjwa hatari utokanao na pombe (Fetal Alcohol Syndrome).

😀Vykulani gani muhimu sana kutumiwa na wajawazito?


✍️✍️Lishe bora wakati wa ujauzito ni muhimu sana, kwani lishe hii hutumika kwa mama na mtoto anaendelea kukua tumboni. kwa kawaida mahitaji ya chakula na virutubisho mwilini mwa mwanamke huongezeka wakati wa ujauzito na kadri ujauzito unavyoendelea kukua, virutubisho hivyo hutumika kujenga mwili wa mama na mtoto. hivyo maamuzi ya lishe au lishe mama anayopata huathiri pia maendeleo ya mtoto anayekua mwilini mwake. tutaona vyakula muhimu vya kuzingatia lishe bora wakati wa ujauzito na baadhi ya vitu vya kukwepa.
Mlo kamili (balanced diet), ni muhimu kwa ajili ya maendeleo mazuri ya afya ya mjamzito na mtoto tumboni. Pamoja na mlo kamili mjamzito hupewa virutubisho ziada (supplements) kwa ajili ya kuongeza madini kama ya chuma na Foliki. Mlo kamili unajumuisha vyakula vya wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji kama inavyochambuliwa hapa chini:
✍️Nafaka na vyakula vya wanga🎯

🎯🎯Vyakula hivi huupa mwili nguvu za kufanya kazi ikiwemo ukuaji wa mtoto tumboni. Vyanzo vya wanga ni kama nafaka mbalimbali(mahindi,mtama,ulezi n.k), viazi, ndizi, mihogo. Ni vizuri mjamzito awe anapata nafaka kamili(whole grains) kama mahindi, ngano na mchele usiokobolewa; cereals n.k.

🎯🎯Nyama, samaki na
vyakula vya protini✍️✍️

Hivi ni muhimu kwenye kuujenga mwili, hasa kipindi cha miwezi wa 4 mpaka wa 9 ambacho viungo mbalimbali vya mtoto vinajengwa. Ni muhimu mama apate vyakula vya protini vya kutosha ili kuhakikisha ukuaji wa mtoto unaenda vizuri. Nyama za kuku, ng’ombe, mbuzi, senene, panzi na wanyama wengine ; vyanzo vya protini za mimea kama maharage, soya, njugu, njegere, karanga,korosho n.k . Samaki, maziwa, mayai ni vyanzo vingine vya protini muhimu

🎯🎯Vyakula vya mafuta✍️✍️

Hutumika kwenye kuupatia mwili nguvu pamoja na ujengaji wa seli za mwili. Mara nyingi vyakula kama nyama, karanga, ufuta, alizeti,senene, panzi, samaki na matunnda kama maparachichi huwa na mafuta. Ni vizuri kutumia mafuta yatokanayo na mimea ili kupunguza mafuta yenye lehemu(cholesterol) nyingi.

🎯🎯Mboga za majani na matunda✍️✍️

Matunda na mboga za majani ni sehemu muhimu sana ya mlo wakati wa ujauzito, kwani huupatia mwili vitamini, madini na kambakamba kwa ajili ya kulainisha chakula. Vitamini husaidia kuimarisha kinga ya mwili sambamba na ufanyaji kazi wa mwili. Madini kama ya chuma, kalsiamu, zinki, madini joto(Iodine) na magneziamu ni muhimu kwa ukuaji salama wa mtoto tumboni mwa mama.Vitamini B9 (Foliki asidi) na madini ya chuma hutolewa kama virutubisho ziada kliniki wakati wa ujauzito ili kutosheleza mahitaji ya mwili na kuzuia hatari ya upungufu wa damu kutokea.

🎯🎯🎯Maji🍉🍉

Maji ni muhimu kwenye mmenyenyo na unyonywaji wa chakula, pia husaidia kuzuia choo kigumu, mwili kuvimba na maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI). Inashauriwa mjamzito anywe maji si chini ya lita 2.3 kwa siku, yanaweza kuwa katika chai, juisi, soda, au maji yenyewe. Ni vema zaidi kama akinywa maji kama maji zaidi na kupunguza vinywaji kama soda.

Mfano wa mpangilio wa mlo

Ili kuhakikisha mlo kamili mjamzito anaweza kufuata mfano wa mpangilio wa mlo ufuatao. Katika mpangilio huu inashauriwa kuchagua aina moja ya chakula kutoka katika kila herufi A mpaka E ili kuweza kuupata mlo kamili.
Mfano:
🍉🍉Mlo wa Asubuhi:🍉🍉
A – Chungwa/ Embe/ Ndizi mbivu/ Parachichi
B – Mkate/ Maandazi/ Chapati/ Vitumbua/ Uji
C – Karoti
D – Mayai
E – Maziwa/ Mtindi/ Siagi/ Maziwa ya Soya

🍉🍉Mlo wa Mchana:🍉🍉
A – Parachichi/ Papai/ Ndizi/ Embe na chungwa
B – Ugali/ Wali/ Ndizi/ Makande/ Tambi
C – Mchicha/ matembele/ Mnavu/ Kisamvu/ Spinach/ Kabeji
D – Maharage/ Samaki/ Kuku/ Njugu/ Nyama/ Dagaa
E – Maziwa/ Mtindi/ Siagi/ Maziwa ya Soya.

🍏🍏Mlo wa Usiku:🍓🍓
A – Parachichi/ Papai/ Ndizi/ Embe na Chungwa
B – Wali/ Ndizi/ Viazi/ Tambi/ Chapati
C – Mchicha/ Matembele/ Mnavu/ Kisamvu/ Spinach/ Kabeji,
D – Maharage/ Samaki/ Kuku/ Njugu/ Nyama/ Dagaa
E – Maziwa/Mtindi/Siagi/Maziwa ya Soya.

DAWA HIZI USITUMIE

HIZI NDIZO DAWA KUMI AMBAZO HAZITUMIKI KABISA KIPINDI CHA UJAUZITO…
✍️Dr .chilo...
🎯🎯🎯💊💊Lakini  bahati mbaya baadhi ya dawa hizo hazitakiwi kupewa kwa wajawazito kabisa kulingana na madhara makubwa yanayoambatana na dawa hizo kwa mtoto aliyepo tumboni.

Zifuatazo ni dawa hizo.


 🎯🎯🎯Albendazole;💝💝

👉👉 hii ni dawa ya minyoo ambayo hutumika mara kwa mara kujitibu lakini ni dawa mbaya sana kwa akina mama wajawazito kwani una uwezo wa kutoa mimba kabisa hivyo mebendazole hutumika kama mbadala.


🎯🎯🎯Gentamycin: 💝💝💝

hii ni dawa ambayo iko kwenye mfumo wa sindano tu, mara nyingi hutumika kutibu magonjwa ya mfumo wa mkojo. Dawa hii huharibu kabisa mishipa ya fahamu kitaalamu kama auditory nerve ambayo hutufanya sisi kusikia. Hivyo matumizi ya dawa hii huweza kusababisha mototo kuzaliwa akiwa hasikii yaani kiziwi.

🎯🎯🎯Ciproflaxin; 💝💝💝

hii ni dawa ambayo hupatikana kwenye mfumo wa vidonge na sindano, mara nyingi hutumika kutibu typhoid, UTI au magonjwa ya njia za mkojo na magonjwa baadhi ya zinaa. Dawa hii huharibu ukuuji wa mifupa ya mtoto na huweza kutoa mtoto asiyetembea mwishoni.


🎯🎯🎯Doxycline: 💝💝💝

✍️✍️hii ni dawa ambayo hupatikana kwa mfumo wa dawa za kumeza kitaaalamu kama capsules, dawa hizi ni antibiyotiki yaani hutumika kuua bakteria wa aina tofauti. Bahati mbaya huweza kuingilia mfumo wa utengenezaji wa mtoto ikitumika miezi mitatu ya mwanzo na kusababisha kuzaliwa na motto mwenye viungo pungufu au zaidi.

🎯🎯Dawa ya mseto ya malaria au ALU;

✍️✍️dawa hii ni salama kipindi chote cha ujauzito isipokua miezi mitatu ya kwanza ambapo dawa hii huweza kuingilia ukuaji wa maumbile ya kwanza ya mtoto[organogenesis} na kutoa motto asiye na viungo vya kawaida.

🎯🎯Metronidazole au fragile;💊💊
👉👉 hii dawa ipo kwenye kikundi cha antibayotiki yaani hushambulia bakteria. Dawa hii hutumika mara nyingi kuua minyoo ya amiba na kutibu magonjwa ya mfuko wa uzazi wa mwanamke na ikitumika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito huingilia mfumo wa utengenezaji wa viungo vya mtoto.


🎯🎯🎯Mesoprostol:💝💝

✍️✍️ hii ni dawa ambayo iko kwenye kikundi maarufu cha prostanglandins analogue, hutumika sana kuongeza njia ya mlango wa uzazi kipindi cha kujifungua na pia hutumika kutibu madonda ya tumboni hivyo matumizi ya dawa hii kipindi cha ujauzito yana madhara makubwa mno ikiwemo kutoa mimba kabisa.

🎯🎯Aspirin: 💝💝

💊💊hii ni dawa ya maumivu ambayo humezwa mara kwa mara na hupatikana kirahisi tu, lakini dawa hii ina uwezo wa kusababisha kuvuja kwa damu nyingi hasa mama akipata matatizo flani ya uzazi kama placenta previa. Sio dawa nzuri sana kipindi cha ujauzito.

🎯🎯Praziquantel: ✍️✍️
💊💊hii ni dawa inayotumika kutibu minyoo flani inayopatikana kwenye sehemu za maji yaliyotuama, ni hatari sana kwa wamama wajawazito kwani huiingilia mfumo wa ukuaji wa mtoto.

🎯🎯🎯Furesamide: 🍎🍎
✍️✍️hii ni dawa ambayo inapatikana kwenye kikundi cha diuretic.. mara nyingi hutumika kushusha ongezeko la maji nje ya mfumo husika wa damu [oedema] na kutibu presha kubwa ya damu. Sio dawa nzuri kwa akina mama wajawazito kwani wajawazito hua na presha ya chini kidogo hivyo huweza kuishusha chini kabisa[intravascular volume depletion].

💓💓💓Mwisho:💞💞💞
✍️✍️✍️ usitumie dawa yeyote kipindi cha ujauzito bila ushauri wa daktari kwani ni hatari sana kwa maisha yako na mtoto wako kwa ujumla...tembelea blog yetu ya kingereza hapa.FSWA

Tuesday, April 14, 2020

CHANGO KWA WATOTO WACHANGA.(COLIC)

TATIZO LA CHANGO KWA WATOTO WACHANGA
Dr.chilo,⚕️ online clinic
💝🤼🤼watoto wachanga wanasumbuliwa na chango(colic) wanapokuwa na umri wa wiki 2 baada ya kuzaliwa ndipo wanapata achango. Chango ni maamivu makali ya tumbo anayopata mtoto na kulia mara kwa mara ikiwa usiku , mchana au jioni ,anaweza kulia zaidi ya msaaa 3 kwa siku usiku .

🌺🌺Chango inachukua muda wa miezi 3-4 ndio mtoto apone kabsa,ingawa sio watoto wote wanapata na tatizo la chango.

🔔 Sababu za kuleta chango kwa mtoto? ✍️✍️
🍓🍓 Maziwa ya ngo’mbe yana protein nyingi , lactose inayopatikana kwenye baby formulas .(hayo yote yanaweza mletea allergy na maumivu ya tumbo)

🍓🍓 Mtoto atakapo nyonyeshwa sana mpaka kuvimbilwa (overfeeding)huchochea chango.
🍓🍓 Hormones-zinachochea mletea maumivu ya tumbo (mtoto akiwa na stress ya mazingira au mama anaposhindwa  kumweka position nzuri wakati wa kunyonya)

🍓🍓  GESI - mtoto ,akiwa analia au kunyonya kwa haraka  anameza hewa inayokuja kuleta gesi na  kumuumiza  tumbo.

🍓🍓 Kiungulia(heartburn)



✍️  Dalili ya chango kwa mtoto (colic)🔔🔔

▶️ Mtoto atalia sana kilio chake kitakuwa tofauti na kile cha kawaida akiwa na( njaa,usingizi , au akiwa kajisaidia n.k).
▶️ Analia sana akijikunja tumbo ,kunyoosha miguu au  vidole ,
▶️ uso utabadili rangi na kuwa mwekundu ,
▶️ pia anaweza kujamba mara kwa mara.

🍒Utamsaidia vipi mtoto💝💝

🌺🌺 Mama unatakiwa kuacha kula baadhi ya vyakula kwa kipindi hiko cha miezi 3-4 ambayo inamsumbua mtoto na chango,kama (kabichi,maziwa yango’mbe au nido, cheese ,kahawa,broccoli,maharage
🌺🌺Baada ya kumnyonyesha mweke begani na mpige pige mgongoni ili abeuwe itamsaidia
🌺🌺 Mama unapo nyonyesha mtoto hakikisha mtoto anaingiza mdomo kwenye chuchu yote na kufunika ule mstari mweusi bila kuacha nafasi akaingiza hewa mtumboni.
🌺🌺 Mfanyie massage ya tumbo- tumia mafuta ya maji weka mkononi sugua viganja vyako vikipata joto mpake tumboni kuanzia juu kuja chini litaletea na gesi zitatoka.
🌺🌺 Weka maji vuguvugu kwenye beseni na mweke mtoto akae kwa dakika 10-15.
🌺🌺 Weka maji vuguvugu kwenye chupa ya plastik funika na taulo mwekee mtoto tumboni(hakikisha -maji yasiwe yamoto sana ukamuunguza.
🌺🌺 Mbebe mtembe tembe au kama kunakiti chake kile cha bembea mweke abembe atanyamaza.
🌺🌺 Mtoe nje apate fresh air.

🌺🌺 Mtoto akilia sana washa  radio inamfanya anyamaze.
🌺🌺 Mbadilishie maziwa ya aina nyingine kama unampa ya kopo(baby formula)
 🌺🌺Usimlishe sana mpaka akavimbilwa(overfeeding)
🌺🌺 Kuna dawa za colic

👩‍⚕️👩‍⚕️ Tiba👩‍⚕️👩‍⚕️
✍️✍️ Kunadawa za  aina tofauti ila usimpe kabla ujaonana na daktari kwani mtoto ni mdogo sana huyo anahitaji uangalizi wa hali ya juu.
👩‍⚕️👩‍⚕️Mtoto akiwa na homa, hayonyi vizuri ,kuhalisha ,degedege muwahishishe kituo Cha Afya kilicho karibu nawe mapema.
🌺🌺TUWALINDE NA KUWALEA WATOTO KWA UPENDO💝💝

Sunday, April 12, 2020

DALILI ZA UJAUZITO

✍️Dr.chilo🌹 online clinic⚕️
👩‍⚕️👩‍⚕️🤰Dalili za ujauzito hutofautiana kati ya mwanamke mmoja  na mwanamke mwingine, ingawa kuchelewa au kukosa hedhi ni dalili moja muhimu sana ya ujauzito Lakini Kumbuka Kukosa hedhi kunaweza sababisha na vitu vingi Sio Mimba tuu..

🌺🌺Ni muhimu kuzitambua na kuzifahamu dalili hizi kwa sababu zinaweza kusaidia kujua kama kweli umeshika ujauzito au la  pamoja na kuweza kutofautisha matatizo mengine yanayoshahabiana kwa dalili na  ujauzito.

Hebu sasa tuangalie dalili na ishara za ujauzito:

🤰Kutokwa damu kidogo ukeni wakati kiumbe kikipandikizwa kwenye mfuko wa uzazi, ingawa siyo wanawake wote hupatwa na dalili hii🌺🌺

🤰Kukosa hedhi, hii ni moja ya dalili kubwa ya ujauzito🌺🌺

🤰Maumivu kwenye matiti na kuvimba matiti (huweza kutokea kati ya wiki ya 1 hadi ya 2)🌺🌺

🤰Uchovu, wanawake wengi huhisi uchovu na  na hali ya kutopenda kufanya lolote.🌺🌺

🤰Kupoteza ladha au kuhisi ladha ya chuma mdomoni🌺🌺

🤰Kuongezeka kwa hisia ya harufu, kipindi cha ujauzito wanawake wengi huongezeka hisia ya harufu🌺🌺

🤰Kichefuchefu na kutapika🌺🌺

🤰Maumivu ya kichwa🌺🌺

🤰Kizunguzungu🌺🌺

🤰Kukojoa mara kwa mara (hasa kati ya wiki 6-8)🌺🌺

🤰Kubadilika rangi kwa ngozi inayozunguka chuchu kuwa nyeusi🌺

🤰Kutamani baadhi ya vyakula na kuchukia vingine🌺🌺

🤰Tumbo kujaa au kuvimbiwa🌺🌺

🤰Kununa na kukasirika haraka au kuanza kuchukia / kuwapenda zaidi baadhi ya watu.🌺🌺

🤰Kiungulia au kupata choo kigumu🌺

🤰Kolostramu kuanza kutoka kwenye matiti 🌺🌺

🤰Kuongezeka uzito🌺🌺

🤰Kuweza kupapasa mtoto (palpation of the baby)🌺🌺

🤰Kulainika na kuvimba kwa shingo ya uzazi (Hegars sign) - kuanzia wiki ya 6

🤰Shingo ya uzazi kubadilika rangi kuwa ya samawati kutokana na msongamano wa damu katika mishipa ya vena. Ishara hii hujulikana kama Chadwick's sign🌺


Dalili nyingine ni pamoja na

🌺Mstari wima mweusi hutokea tumboni kuanzia chini ya kitovu (linea nigra)💖💖

🌺Mama kuhisi mtoto akicheza (kuanzia wiki ya 20)💖💖

🌺Maumivu ya mgongo hasa mimba ikishakuwa kubwa.💖💖

🌺Kipimo cha mimba kuwa chanya (positive).💖💖

🌺Kusikia mapigo ya moyo ya mtoto💖

🌺Mtoto kuonekana kwenye kipimo cha ultrasound💖💖

💞💞KUMBUKA kupika kituo Cha Afya mapema pale unapohosi unaujauzito.
✍️✍️ ASAAAAAAANTEEE.
TOA MAONI HAPO CHINI

Saturday, April 11, 2020

JE UKIJIFUNGUA LINI UANZE KUFANYA TENDO LA NDOA?JIBU HILI HAPA

💞💞 hili swali wanawake wengi hujiuliza baada ya kujifungua, lini nianze kumpa Utamu???? lakini kitaalamu ni kwamba uwe umezaa kwa upasuaji au kwa njia ya kawaida hutakiwi kushiriki tendo la ndoa mpaka wiki sita ziishe na wiki sita sikishaisha wewe mwanamke unaweza kujitafakari kama uko tayari au bado kwa ajili ya tendo hilo yaani kwa sababu za kisaikolojia zaidi yaani uchovu na msongo wa mawazo.

je kwanini sio vizuri kushiriki tendo la ndoa kabla ya wiki ya sita?

💞maumivu kipindi cha tendo la ndoa;
 hii husababishwa na mabadiliko makubwa ya viwango vya homoni mwilini hasa kupanda kwa homoni ya kutoa maziwa ya mama kitaalamu kama prolactin na kushuka kwa homoni za uzazi yaani progesterone na eostrogen, hii inaweza kusababisha uke kuwa mkavu sana na kuleta maumivu wakati wa tendo.
nini cha kufanya? muuleze kistaarabu mpenzi wako kuhusu hili na aelewe kwamba ukavu wako hausababishwi na kupungua kwa mapenzi yako kwake, lakini hata baada ya wiki ya sita ukavu huu unaweza kuendelea hivyo mnaweza kutumia vilainishi kama ky gel kusaidia hili.
🌹ladha ya tendo la ndoa haitakua kama mwanzo;🌺🌺
hii ni sababu ya kupanuka sana kwa misuli ya uke hivyo mwanamke anakua hausikii vizuri uume kama mwanzo na unaweza kuona kama hakuna ladha tena.
nini cha kufanya?
fanya mazoezi ya kegel, mazoezi haya yaligunduliwa na doctor arnord kegel mwaka 1948 ambaye alikua bingwa wa magonjwa ya kina mama yaani obstretic and gynacology specialist..mazoezi haya hufanywa kwa kubana msuli ambao unautumia kuzuia mkojo wakati wa kukojoa, sasa bana msuli huu wakati hauna mkojo kwa sekunde kumi na kuachia kwa sekunde kumi...fanya mara tatu asubuhi mchana na jioni na uke wako utarudi kua mdogo kama zamani.

💞matiti baada yanatoa maziwa mengi;

 hii inaweza ikafanya tendo la ndoa lisiwe la furaha sana hasa wakati mwanamke anafika kileleni maziwa yanaweza kumwagika mengi sana na hii pia inaweza kuendelea mpaka zaidi ya wiki ya sita sababu mtoto anakua bado anaendelea kunyonya na hata usipompa titi maziwa yataendelea kutoka.
nini cha kufanya? jitahidi kuvaa sidiria nzito wakati wa tendo la ndoa kuzuia hali hii ambayo inaweza isiwe nzuri hasa kwa mwenzi wako.

🌹🌹huna amani na mwili wako; 💝💝
huchukua mpaka miezi miwili kwa tumbo la uzazi kurudi kwenye hali yake ya zamani. yaani mtu akizaa anakua bado anamuonekano wa mtu mwenye ujauzito wa miezi sita, na kurudi kwenye uzito wa zamani inaweza kuchukua mpaka mwaka mmoja kama ukifanya mazoezi na usipofanya unaweza kubaki vilevile au kuongezeka.[watanzania wengi hawafanyi mazozi baada ya kuzaa na hunenepa zaidi]
nini cha kufanya?
usiwe na wasiwasi sana kwani mume wako anaelewa mabadiliko ya mwili wako yanasababishwa na uzazi, lakini pia penda ulichokipata kwani mpaka umepata huyo mtoto umepitia mateso makubwa ya jasho na damu. kikubwa anza mazoezi pale utakapokua tayari.

💝💝kuna hatari ya kubeba mimba nyingine ?;

 Ndio ,japokua uwezekano wa kubeba mimba nyingine baada ya kujifungua hua ni mdogo sana lakini sio kwamba haiwezekani kabisa kwani mimi binafsi nimekutana na watu waliobeba mimba kipindi hiki. hii ni sababu ya kuchelewa kuanza kuona siku zako za hedhi na kutoona siku zako kunaweza kukufanya ushindwe kuhesabu siku zako za  hatari.

💞vidonda bado havijapona;💞
 kama ulizaa kwa upasuaji au njia ya kawaida bado kuna vidonda ndani ya uke na uzazi ambavyo vilisababishwa na mtoto kupita ukiachilia mbali kidonda cha upasuaji ambacho mara nyingi hua hakina hali nzuri kabla ya wiki ya 6. hivyo ukishiriki tendo la ndoa unaweza kusababisha magonjwa yaani infection na kuugua, kusabaisha kuachia kwa mshono wa upasuaji au kuhatarisha afya ya kizazi kwa ajili ya watoto wajao.
nini cha kufanya?
mueleweshe mume wako kuhusu uwezekano wa kupata magonjwa na atakuelewa.

🌹🌹mwisho;🌹🌹
hali hii ni ya muda tu, wewe kama mwanamke kua mstari wa mbele kuhakikisha unapona mapema na kurudi katika hali yako ya zamani, ndoa nyingi huanza kuharibika hapa kwani wanawake hutumia nafasi hii kuwanyima unyumba waume zao kwa muda mrefu sana kwa kisingizio cha uzazi huku wakisahau kwamba huko nje kuna wakware wanasubiri ushindwe huku ndani wambebe mumeo.

🌺🌺 ASAAAAAAANTEEE 💞💞
KURUDI KWENYE UBORA BAADA YA KUZAA INAWEZEKANA ?💖💖
toa maoni yako hapo chini.

EPUKA TUMBO BAADA YA KUJIFUNGUA,FANYA HIVI

NJIA RAHISI KUMI ZA KUPUNGUZA TUMBO BAADA YA KUJIFUNGUA.


✍️✍️baada ya kujifungua wanawake wengi hujikuta bado wana matumbo makubwa yaani wakati mwingine watu wasiokujua wanaweza wakahisi bado haujazaa, lakini ukweli ni kwamba inakuchukua miezi tisa kulivimbisha tumbo hilo hivyo hata kulipunguza huchukua muda fulani.
                                                                          
kwa kawaida kizazi kinachukua wiki mbili kurudi hali yake ya kawaida lakini mafuta yaliyoko eneo la tumbo yawezi kuondoka  kirahisi kama usipochukua hatua yeyote.
                                                                    
kitu gani kinafanya mwanamke apate tumbo baada ya kujifungua?
kwa kawaida mwanamke huongezeka kilo 12 akibeba mimba hii ni kutokana na uzito wa mtoto, uzito wa  kondo la nyuma na ulaji wa chakula ambao mtoto anauhitaji sana ili kukua lakini baada ya kujifungua mama  hupunguza kilo sita tu na  kilo sita zingine hubaki kama mafuta eneo la tumbo.

inachukua muda gani hasa kwa tumbo la uzazi kuondoka?
baadhi ya wazazi huchukua siku kadhaa, baadhi huchukua miezi kulingana na bidii ya mwanamke husika ya kulitoa tumbo baada ya kujifungua.

mambo ya kuzingatia ili kuliondoa tumbo la uzazi...
🌺🌺nyonyesha mtoto
 kunyonyesha mtoto sio kuna ongeza kinga ya mtoto tu lakini kunasababisha kuongezeka sana kwa homoni ya oxytocin ambayo inahusika na kupunguza ukubwa wa kizazi na kuzuia homoni za uzazi ambazo zinahusika na kuongeza ukubwa wa kizazi wakati mwanamke ana mimba.
wanawake wengi wa siku hizi hawanyonyeshi kwa sababu za kiurembo lakini nakwambia wengi wao huishia kua wanene sana kwa kukosa faida hii.

🌺vaa / kitambaa mkanda wa tumbo
; hii ni njia ya kiasili na kizamani zaidi kwani imetumika kwa miaka mingi na watu wa rangi mbalimbali duniani.
mkanda wa tumbo husaidia kuikaza misuli ya tumbo na kuongeza kasi ya kupungua kwa ukubwa wa kizazi.
ukiwa unavaa mkanda wa tumbo au unafunga kitambaa chochote hakikisha haukazi sana au kulegeza sana ili uweze kupata matokeo mazuri.
Funga mkanda kwa masaa 3 hadi 4 kisha fungua kufanya mwili uwe huru .
kwa matokeo mazuri zaidi, mkanda huu uvaliwe kwa  wiki nne mpaka sita baada ya kujifungua.
🌺🌺fanya mazoezi;
 mazoezi husaidia sana kupunguza tumbo la uzazi, sio lazima kufanya mazoezi mazito sana lakini unaweza kutembea, kukimbia kidogo, kuruka kamba,cardio na kadhalika, na utapata matokea mazuri sana ndani ya muda mfupi,
fanya mazoezi angalau dakika 20 mpaka 30 kwa siku hasa pale mtoto anapokua amesinzia.

✍️✍️kuwa uangalifu na epuka diet kali sana; 🍒
wanawake wengi hupaniki baada ya kuzaa na  huanza kufunga kula na kuruka chakula ili wapungue haraka kitu ambacho sio kizuri kwako na kwa mtoto.
kipindi hiki bado unahitaji chakula cha kutosha ili uweze kupata maziwa mengi ya kumpa mtoto, hivyo punguza sana ulaji wa vyakula vya wanga kama ugali, mihogo, wali, ndizi na acha kabisa kula wanga ambao sio muhimu kama chips, sukari, biskuti, soda,maandazi, na fast food zote.
kula zaidi vyakula vya protein kama nyama, samaki, dagaa, maharage na karanga huku ukichanganya na mboga za majani na matunda kwa wingi.
kumbuka ni vizuri kula kidogo kidogo angalau mara sita kwa siku kuliko kula milo mitatu mizito.
🌺🌺pumzika; 👍
ni kweli mtoto hua anasumbua sana lakini mtoto akitulia na wewe pumzika ili upate usingizi wa kutosha.
kwa hali ya kawaida kama mama hupati usingizi mwili wako unakua katika hali ambayo sio ya kawaida, hali hii huvutia mafuta katikati ya tumbo na kukufanya uendelee kua mnene.

kunywa chai ya kijani[green tea]; majani haya yamejizolea umaarufu duniani kote kwani huondoa sumu mwilini na kusaidia sana kwenye uchomaji wa chakula kwenye mwili wa binadamu.
kwa kutumia majani ya chai haya kila siku hukusaidia sana kupunguza kitambi cha uzazi.
                                                          
kunywa maji ya uvuguvugu; kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi na hata mchana ukisikia kiu, unaweza kuchanganya na limao kidogo.
maji ya uvuguvugu huongeza kasi ya uchomaji wa mafuta ya mwili kwa kuongeza joto na kuondoa nje sumu ya mwili.

💝epuka msongo wa mawazo; 

msongo wa mawazo humwaga homoni aina ya cortisol kwenye damu ya mtu, homoni hiii husababisha kuchoka  na kuongezeka uzito.
hakikisha mambo yako umeyapangilia vizuri na hata kama kuna kitu unaona kinakupa mawazo sana basi usikipe nafasi, amini matatizo yapo kwa kila mtu na yataisha tu.
kua majani nyingi; 

mboga za majani husaidia mmengenyo wa chakula, huondoa sumu ambazo zinajikusanya kwenye utumbo mkubwa, pia zina virutubisho vingi na uzito mdogo[calories] kiasi kwamba hata ukila nyingi haziwezi kukunenepesha...hii husaidia kupunguza uzito.
                                                                        
                                                              
mwisho;hakuna uzazi rahisi, mara nyingi ukijifungua lazima uongezeke uzito..hivyo ni wajibu wako kupambana na uzito huo mpaka urudi kwenye hali yako ya kawaida.
kuendelea kua mnene baada ya kujifungua kuna madhara mengine baadae ikiwemo kisukari, shinikizo a damu, ugonjwa wa moyo na uzazi mgumu wa mimba zijazo..

Tuesday, April 7, 2020

TUNZA KITOVU CHA MTOTO HIVI ,NI MUHIMU SANA

 JE MAMBO MUHIMU YA KUTUNZA KITOVU CHA MTOTO

✍️Dr.chilo.#online clinic⚕️
👩‍⚕️ MwanaApp ♥️

Kitovu cha mtoto kinatakiwa kuangaliwa kwa umakini Baada ya kukatwa,haswa Unapo  mbeba ,kusponge (mpangusa kwa Maji)na kumvesha diaper au nepi! kinachukua siku 4-7 kuanguka inategemea mtoto na mtoto !kina kuwa kinabadili rangi toka njano-kijani-kahawia-nyeusi hapo tayari kuanguka!
⚠️⚠️
1:usimwache tumbo wazi!

2.hakikisha yupo mkavu MUDA wote!

3:usi mwogeshe mpaka kitovu kikatike mpanguse na kitaulo cha maji hakikisha  hakuna Maji yanavyo pita Kwenye kitovu! Au
Kama una uzoefu  wa kumwogesha unaweza mwogesha
Ila HAKIKISHA Maji yasiingie  Kwenye kitovu!

Hii itamsaidia kutopata infections

🔔DALILI HATARISHI ZA KITOVU!

✔️mtoto anapata joto sana na kuvimba au kuvilia damu maeneo YA kitovu! ✔️unjano kama unaotunga  usaha

Na kitovu kutoa harufu !

Ukiona HIZO dalili wahi hospital! ⚠️⚠️swala la kitovu kuanguka sehemu YA uume na mtoto  kutokuwa rijali  sidhani kama ina ukweli wowote ni imani tu ?
🌹🌹hii ilikuwa na lengo la kumfanya mama awemakini zaidi na kitovu Cha mtoto , hakuna mwanamke anaependa mtoto wasiwe rijari.

💋💋KITOVU NI SEHEMU MUHIMU SANA KATIKA AFYA YA MTOTO✍️

Monday, April 6, 2020

ZUIA MIMBA BAADA YA TENDO LA NDOA


 
✍️Dr.chilo
🤰🤰 Unaweza kuzuia Mimba  kwa kutumia Dawa ya emergency pill, maarufu kama P2 zimekuwa zikitumika sana kwa wanawake baada  ya kuhusika kwenye tendo la kujaamiiana bila kinga ama kondom kupasuka, kwa lengo la kuzuia na kuepuka mimba.
💋💋Hupatikana madukani pia kwa majina mengine, likiwemo PLAN B. Kiambata hai katika dawa hizi ni homoni ya Levonorgesterol. 
⚕️⚕️UFANYAJI KAZI  WA P2👩‍⚕️
✍️✍️Dawa hii hufanya kazi yake kwa, aidha, kuzuia mbegu ya kiume isifikie yai la kike ili kutunga mimba (kuzuia fertilisation), kupunguza uwezo wa mfuko wa uzazi (uterus) kuhudumia yai lililochavushwa na mbegu ya kiume (kuzuia implantation au kupandikizwa kwa mimba) au kuzuia yai la kike lisitoke katika ovari ili kuchavushwa (kuzuia ovulation).
👩‍⚕️JINSI YA KUTUMIA P2.🌹🌹
Dawa hii hutakiwa kutumika tu kama njia ya dharura na sio njia ya uzazi wa mpango, yaani ,isitumike mara kwa mara. Ufanisi wake katika kuzuia mimba ni ndani ya masaa 72 toka tendo la kujamiiana limefanyika. Masaa 24 huaminika kuleta ufanisi wa hadi asilimia 98/99.Inapotumika mapema zaidi ndivo nguvu ya kufanya kazi inakuwa kubwa zaidi.
📌📌Matumizi ya dawa hii hayawezi kuondoa ujauzito uliopo tayari au kuzuia magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana kama UKIMWI, kisonono, kaswende, n.k
👩‍⚕️👩‍⚕️ MADHARA YAKE NII👩‍⚕️👩‍⚕️
✍️ ni kama vile kujisikia vibaya, kichefuchefu na kuhisi kutapika, pia hubadilisha mzunguko wa hedhi na kupelekea hedhi kuja mapema zaidi au kuchelewa. Hedhi inaweza kuwa nzito au nyepesi kuliko kawaida.
⚕️⚕️Dawa hii inashauriwa na wataalamu wa afya kuwa itumike si zaidi ya mara 3 kwa mwaka kwani baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa matumizi ya mara kwa mara ya dawa hizi yanaweza kupeleka mtu kupata saratani, kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi kutokana na kuvurugika kwa viwango vya homoni (vichocheo) na kuathiri vitu vingine vinavyotegemea vichocheo hivyo.
🤰🤰Kuliko kutumia dawa hizi mara kwa mara ni vizuri kutumia njia zilizo salama zaidi  ili kuepuka ujauzito kama kufahamu mzunguko wa hedhi, kutumia kondomu n.k
💋💋 Asante cheza salamaa👩‍⚕️
🌹Toa MAONI yako hapo chini✍️

Saturday, April 4, 2020

STAILI TAMU NA SALAMA

😍STAILI TAMU ZA KUFANYA MAPENZI KIPINDI CHA UJAUZITO.💯

💃💃Jinsi ya kufanya mapenzi wakati wa ujauzito
Bila shaka kila aliyeko kwenye mapenzi ana kiu yakufahamu staili mbalimbali atakazotumia katika uwanja wa UTAMU 😋 kumpagawisha mwenza wake, kimsingi kuna staili nyingi sana ijapokuwa nyingi huhitaji wapendanao wawe wanasarakasiyaani wawe wepesi wa viungo.
🍎🍎Leo nitazungumzia staili MBILI ambazo mwanamke mjamzito anaweza kutumia na mwenza wake wakiwa katika 6 KWA 6  na kumfanya afurahie tendo la ndoa na
panapomajariwa nitazungumzia staili nyingine ambazo kila mmoja wetu anaweza kutumia  ukiwa anajibabishaa kumpagawisha mwenza wake.

🤰🤰DOGGY STYLE: 😋😋
💓💓hii ndo mama lao Sasaaa utapata kuwehuka kwa raha Utamu Yan unafanya kumsusia mwanaume loooo🍎🍎
Hapa mwanamke anapaswa kUINAMA AU KUPIGA MAGOTI na kushikilia ama kiti, kitanda au kitu chochote kitakachomfanya asichoke miguu yake wakati mwanaume atakapokuwa akimwingilia kimwili akiwa nyuma kasima Kama ng'ong'otiii yaan anakutekenya tekenya. Hii ni staili nzuri kwa mwanamke mjamzito kwani mwanaume huweza kusikia raha ya tendo na kuigusa G-Spot vizuri itawapa raha wote
na kumbuka mwanaume hatakiwi kuingiza DU""DU kwa kasi kama unakimbizwa kama mama ashafikisha miezi sita .

💋💋SPOON/KIJIKO STYLE: 💞

👁️‍🗨️👁️‍🗨️hapa mwanamke hujilaza kwa
ubavu na kukunja miguu yake kidogo ili uke uwezekujitokeza nje vizuri zaidi hapa mwanaume anatakiwa naye awe amejilaza kiubavu  Hivi ili kuruhusu DU""DU  kuingia ndani vizuri na bila ya kumuumiza kiumbe kilichopo tumboni
hapa pia mwanaume hutakiwa kwenda pole pole  Kama anaisusa Hivi kumbe imooooooh na style hii humfikisha mwanamke mjamzito kileleni na ni nzuri kwa mama mjamzito miezi 5+

📌📌MUHIMU:

💋💋Ni kweli katika kipindi cha ujauzito wanawake wengi hujisikia kuchokachoka sana hali inayowafanya wasipende kushiriki tendo la ndoa na imani potofu et sio VIZURI Kushiriki TENDO  lakini hali huwa tofauti kwa wanaume wengi pindi wapenzi wao wawapo wajawazito kwani ni kipindi ambacho mwanaume hufurahia sana kushiriki tendo la ndoa na mjamzito kutokana 💞na ukweli kuwa katika kipindi hiki mwanamke huwa na joto lakutosha sehemu zake za siri, joto ambalo humfanya mwanaume apagawe
na kusikia raha hatareee 💯💯 hatamani Kutoka.
🤰🤰Hivyo mjamzito anapaswa kuhakikisha anafanya kila analoweza kumpa mwenza wake unyumba.
👩‍⚕️👩‍⚕️ISIPOKUWA  tu endapo atakuwa ameshauriwa na daktari kutoshiriki tendo la ndoa kwa sababu za kitaalam!


💞💞💞ILA kama hakuna zuio nasema mpe mpe mumeo penzi zito na joto ulilonalo utamfanya asichepuke Hivyo itakuwaka Salama na kuambukizwa magonjwa hatari.mpe kwa style utakayoona unampagawisha bila kumuumiza mtoto.
🌹🌹 Toa maoni na share kwa wengine.
👩‍⚕️👩‍⚕️Dr.chilo,
💓💓 online clinic.

🍎 JE WAZIJUA FAIDA🔟 ZA KUFANYA MAPENZI KIPINDI CHA UJAUZITO?


✍️DR.CHILO

Kuna watu wamekua wakiuliza mara kwa mara kama inaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa mpaka umri gani wa mimba au ni sahihi kufanya tendo la ndoa kipindi cha ujauzito?

✍️Mwanamke akiwa na mimba anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa hata kama anatarajia kuzaa kesho yake, hakuna tatizo lolote linalomzuia kufanya hivyo, baadhi ya wanawake wamekua wazito sana kufanya hivyo kwa kua na sababu mbalimbali za kujitetea bila kujua kwamba wanazikosa faida hizi ambazo ni muhumu kiafya.faida zenyewe ni kama zifuatazo:

1️⃣Husaidia uchungu mzuri na kupona mapema;😍
 kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa huambatana na kubana kwa misuli ya nyonga hii husaidia kuweka imara misuli ya nyonga ambayo ni muhimu sana wakati wa kusukuma mtoto na baada ya kuzaa kwani misuli hii ikiwa legevu mwanamke huweza kushindwa kuzaa kwa njia ya kawaida na hata baada ya kuzaa huweza kushindwa kuzuia mkojo usitoke wenyewe au kuvuja damu kwa muda mrefu.

2️⃣Hupunguza kwenda ovyo kukojoa au kujikojolea🤰🤰
💓; wakati wa ujauzito mtoto anapozidi kua mkubwa anazidi kukandamiza kibovu cha mkojo, hii humfanya mama aende chooni kukojoa mara kwa mara na wakati mwingine hata akipiga chafya au kukohoa basi mkojo unaweza kutoka wenyewe. tendo la ndoa huibana misuli ya nyonga na kuzuia hali hii.

3️⃣Huzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba;🌹
🔔 tafiti zinaonyesha kwamba aina ya protini inayopatikana kwenye mbegu za mwanaume huongeza kinga ya mwili na kuzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba ambacho kinaua wanawake wengi sana.

4️⃣Hutibu tatizo la kufika kileleni kwa shida;🤔🤔
🌹🌹 kipindi cha ujauzito chuchu za mwanamke na kinembe chake huvimba na kuongezeka hisia mara dufu huku kiwango cha homoni za oestrogen kikiwa juu sana, hii humfanya kufika kileleni kirahisi sana kuliko mwanzoni kwa Sababu uke Kipindi hichi huwa na joto kuliko mwanamke asaie na mimba.5️⃣HUWAPA UWEZO WA KUJIAMI NA KUJIKUBALI.💪
;🤰🤰 kipindi cha ujauzito mwanamke hua anapata hofu sana na kutojiamini na mwili wake, hua na wasiwasi kwamba mwili wake unaharibika hivyo kitendo cha mwanaume wake kuendelea kushiriki naye tendo la ndoa humpa kujiamini kwamba mwili wake bado uko kwenye hali nzuri na anapendwa.kipindi Cha UJAUZITO MWANAMKE anakuwa mtamu ZAIDI.

6️⃣Hupunguza msongo wa mawazo;📌 🌷🌷kipindi cha ujauzito wanawake wengi huwaza sana kuhusu kesho yao...je swala la uchumi litakuaje? mwili wangu utakuaje? je nitapata jinsia nayotegemea? na kadhalika.. tendo la ndoa hutoa homoni ya upendo kwa jina la oxytocin(hormone of love), homoni hii hupunguza mawazo na kumpa amani mjamzito.

7️⃣Huongeza upendo na mshikamano kati ya wapenzi;💓💓

🤰🤰 katika hali ya kawaida wanandoa wakikwazana wanaweza wakapatana kwa kushiriki tendo la ndoa tu, amani na upendo kipindi hiki ni muhimu sana kwani kuna mtoto anakuja ambaye anatakiwa kuzaliwa huku baba na mama wakiwa wanapatana na kupendana.

8️⃣Hukuandaa na uchungu;🌶️🍎

🍇🍇ukishiriki  TENDO LA ndoa wakati wa tarehe zilizokadiriwa zimefika unapata homoni moja kutoka kwenye mbegu za mwanaume kwa jina la prostglandin, homoni hii huivisha mlango wa uzazi na kuanza kufunguka taratibu kujiandaa na uchungu.

9️⃣Hutibu tatizo la kukosa usingizi;🙄 🍎🍎wanawake wengi wajawazito hua na dalili mbalimbali za maumivu na kuumwa sehemu tofauti za mwili na msongo wa mawazo, hii huweza kuwakosesha usingizi kabisa..tendo la ndoa huweza kuwapa usingizi mzuri Sana pale watakapofikishwa kileleni.

🔟Hupunguza presha ya damu;🚑🚑
💃💃 kipindi cha tendo la ndoa presha ya damu hushuka kwenye kiwango kizuri sana, hii ni muhimu sana kwa wanawake wenye hatari ya kupata kifafa cha mimba kama wanene sana, wenye kisukari au wenye historia za ugonjwa wa presha kwenye koo zao.

🌹🍎Hakikisha unatumia staili za tendo la ndoa ambazo hazimuumizi mtoto na mama yaani hakikisha haulilalii tumbo hasa mimba ikiwa kubwa,
🛌👌 kuna staili muhimu kipindi hiki kama kuangalia upande mmoja, mwanamke kukaa  juu ya Mpenzi wake, au mwanamke kuinama
😍😍Kama nawaona mnavyopata rahaaa vile mmwaaaaaaaaah 😘😘
nawapenda Sana.
🍎🍎KAMA UTASHAURIA NA DAKTARI KUTO KUFANYA TENDO LA NDOA NAKUOMBA UFATE USHAURI HUO.
✍️Dr.chilo.
🍎✍️ online clinic⚕️ MwanaApp ♥️

🤰🤰MAZOEZI KIPINDI CHA UJAUZITO!!🍎🌺


✍️Dr.chilo.💓 online clinic⚕️

🌹🌹 Kawaida ujauzito kwa mwanamke hudumu ndani ya wiki 40 ambapo kwa jumla ni sawa na miezi tisa. Ndani ya kipindi hicho mwilii wa mwanamke hupata mabadiliko mengi,hutokana na ukuaji wa mtoto ndani ya tumbo la uzazi. Mabadiliko hayo ndani ya mwanamke mjamzito kwa kitaalamu hutokea kwa vipindi vitatu ambavyo ni;
1️⃣ Kipindi cha kwanza (first trimester)
2️⃣ Kipindi cha pili( second trimester),
3️⃣ Kipindi cha tatu( third trimester).

🤰🤰 Ni ndani ya vipindi hivi ambapo mtoto huchukua hatua ndogo ndogo za ukuaji na vipindi hivi hufahamika kulingana na wiki ambazo mwanamke mjamzito amezifikisha.
🍎🍎Ni kweli kwamba kuna haja kubwa ya wanawake wajawazito kufanya mazoezi kutokana na kwamba miili yao huitaji kuwa na nguvu na imara ili afya ya mtoto iweze kuimarika vyema.

🤰Faida ya wanawake wajawazito kufanya mazoezi ni kwamba 
👍👍Ukuaji wa mtoto ndani ya mama mjamzito huleta mabadiliko katika mfumo wa mwili wa mwanamke kwa namna nyingi kama vile.
🌷🌷Uvutaji pumzi,
🌷🌷Mzunguko wa damu,
🌷🌷Mapigo ya moyo
🌷🌷Mpangilio wa misuli ndani ya mwili wake.
🌷🌷mfumo wa Hormone
🌷🌷Hadi mfumo wa tabia.

🔔🔔Mazoezi kwa wanawake wajawazito hupaswa kufanywa kwa kuzingatia vipindi vitatu vya ujauzito kama nilivyo elezea awali.
🌺🌺Ndani ya vipindi hivyo vitatu mwanamke mjamzito anapaswa kufanya mazoezi kulingana na kipindi alichopo ili aweze kupunguza uwezekano wa majeraha kutokana na mabadiliko yaliyoletwa na ujauzito pia kuepusha kuhatarisha maisha ya mtoto.

1️⃣💓Kipindi cha kwanza(first trimester)
Hutokea kwanzia pale mtoto anapotungwa tumboni mwa mama yake mpaka wiki ya 12. Ndani ya wiki hizo kumi na mbili ndipo mgongo na ubongo huanza kujitengeneza kwa mtoto tumboni na pia misuli inayotengeza umbo lake huanza kuonekana.Mwanamke mjamzito ndani ya wiki hizi kumi na mbili asiye na historia ya kufanya mazoezi  anashahuriwa kufanya mazoezi ya kawaida  kama vile;
🤰🤰●Yoga🌺🌺
Ambapo atanyoosha misuli ya mwili na kumfanya ajisikie vizuri na mwenye afya, zoezi hili maranyingi hufanyika kwa kukaa chini na sehemu tulivu. Japo unaweza fanya sehemu yoyote.

🤰🤰●Kutembea.🌹🌹

Ambapo kwa kutembea kutamfanya aweze kupunguza uwezekano wa mwili wake  kuvimba kwa kukaa sehemu moja na pia kujenga pumzi.

🤰🤰Kucheza aerobics🍎🍎

Kwa kufanya mazoezi ya aerobics kutamwezesha kufanyisha moyo mazoezi kwa  kusukuma damu kwa wingi,pia  kutamsaidi  kutokuvimba kwa mwili. Mazoezi haya unaweza kufanya kwenye ngazi au kitu chenye mfano wa ngazi, unakuwa unapanda na kushuka kwenye ngazi hiyo moja tu.
Kwa mwanamke mwenye uzoefu katika ulimwengu wa mazoezi anaweza akafanya mazoezi zaidi kuliko mwanamke ambaye hana historia ya kufanya mazoezi. Mazeozi ya nyongeza ukitoa yale ambayo mwanamke asiye na historia ya mazoezi anayoweza kufanya ni kama vile;

🤰🤰Squat🍎🍎

Ambapo kwa kufanya hili mwanamke mja mzito mwenye uzoezi wa mazoezi anaweza   akajenga nguvu zaidi ya miguu.
Mazoezi haya hufanyika kwa kutanua miguu kiasi kasha unakuwa kama unataka kuchuchumaa lakini hufiki chini, huku mikono yako unanyoosha mbele, fanya hivyo kwa kwenda chini na juu. angalau dakika 15  tu usifanye mazoez Hadi uchoke Sanaa,hii Husaidia  Miguu isivimbe na kufangazi.

🤰🤰Kuogelea🏊🏊

kwa kufanya mazoezi ya kuogelea mwanamke mjamzito anaweza kuongeza nguvu ya viungo vyake vya mwili na pia kujenga pumzi .

2️⃣Kipindi cha pili (second trimester) 🤰

🤰🤰Kipindi hiki hutokea kunzia wiki ya 13 na humalizika hadi wiki ya 27.
Ndani ya kipindi hiki ndipo mtoto anapoanza kuongezeka misuli ya mwili wake, ngozi yake huanza kuonekana na pia mwili wa mtoto hukua hadi inch 4 mpaka 5. Mwanamke mjamzito ndani ya kipindi hiki huonekana kuwa na tumbo kubwa kidogo ukilinganisha na kipi cha kwanza, na pia mazoezi anayopaswa kufanya ni machache ukilinganisha na mazoezi ya kipindi cha kwanza.
Mazoezi anayoweza kuafanya mwanamke mjamzito ndani ya kipi hiki ni;
📌📌Mazoezi ya kujinyoosha.

Kwa kufanya mazoezi ya kujinyoosha(stretching) kunaweza kuweka mwili  wake katika hali nzuri ambapo hatopata maumivu ya viungo kama vile mgongo na mengineyo.

🤰🤰●Kutembea💃💃

Kwa kufanya mazoezi haya ya kutembea kunaweza kumsaidia mjamzito kutokuvimba kwa miguu yake na pia kusaidia kwenye suala la pumzi.

🌺🌺●Yoga
Kutokana na ukubwa wa tumbo kwa kipindi hiki na kushindwa kufanya mazoezi mengi kwa mama mjamzito basi ni vyema kufanya zoezi hili ili aweze kujinyoosha na kutengeneza afya  ikawa poa.

3️⃣Kipindi cha tatu(third trimester) 🤰🤰

kipindi hiki huanzia kutoka wiki ya 28 na humalizikia wiki ya kujifungua. Ndani ya kipindi hiki ndipo mwanamke mjamzito hula sana kutokana na kwamba umalizikiaji wa ukuaji wa mtoto tumboni hutokea.
🍎🍎Kipindi hiki ndipo mwanamke mjamzito anapaswa kuwa mwangalifu ambapo atapaswa kupunguza kazi nyingi na mazoezi mazito, na hivyo anapswa kufanya mazoezi marahisi.
Mazoezi ambayo anayoweza kufanya mwanamke mjamzito kwa kipindi hiki ni;
●Kutembea💃💃
Mwanamke mjamzito ndani ya kipindi hiki hushauriwa sana kufanya mazoezi ya kutembea kwa umbali mdogo ili aweze kupunguza uwezekano wa kuvimba miguu yake na pia humsaidia kwenye suala la pumzi.

●Mazoezi ya kujinyoosha
Kwa kufanya mazoezi ya kujinyoosha(stretching) kwa mwanamke mjamzito wa kipindi hiki cha mwisho kunaweza kumsaidia mwili wake kwa kuuweka katika hali nzuri ambapo hatopata maumivu ya viungo kama vile mgongo na mengineyo.

🤰🤰HITIMISHO 📌📌
 FANYA mazoezi kwa kiasi ,na jiepushe na kunywa pombe , Uvutaji wa sigara na migogo isiokuwa ya lazi na watu wako wa karibu ,
🤰🤰 Dr.chilo .💓NINA WAPENDA SANA.MUNGU ATIMIZE HITAJI LA MOYO WAKO.
📌📌TOA MAONI HAPO CHINI.