Monday, March 23, 2020

SABABU NA DALILI ZA MIMBA KUTOKA YENYEWE

[🎯 JE WAJUA VISABABISHI VYA  KUHARIBIKA KWA MIMBA🌹🌹 {Miscarriage}?
Kuharibika kwa mimba ni janga kwa wanawake wengi siku hizi,na kama bado unajiuliza nini sababu za mimba kutoka,soma hizi hapa utaelewa;
⬇️1.Chromosome abnormalities,
mimba nyingi ambazo huharibika hadi wiki ya ishirini husababishwa na tatizo hili la chromosomes, na chromosomes huwa zinabeba genes ambazo huyatambulisha maumbile ya mwanadamu kwa nje, yaani jinsia yake, ngozi yake itakuaje, macho yake na vitu vingine vingi nisingependa tuingie ndani sana lakini matatizo haya ya chromosomes huchangia sana kuharibika kwa mimba.

⬇️2.Maambukizi katika mji wa uzazi wa mwanamke {Infections}
kuna kitu kinaitwa Pelvic Inflammatory Diseases {PID} yaani kuvimba kwa kuta za mji wa mimba au kuvimba kwa mirija ya uzazi nayo pia huchangia sana kuharibika kwa mimba kwa mwanamke, lakini pia Candida au fangasi nazo pia huchangia sana kuharibika kwa mimba.

⬇️3.Chanzo kingine kikubwa ni utoaji wa mimba
Utoaji wa mimba wa mimba za mara kwa mara, wanawakie au wasichana wenye tabia ya kutoa mimba moja au mbili au tatu basi nao pia hukutwa na tatizo hili la kuharibika kwa mimba kwani uingizaji wa vyuma ndani huweza kuharibu shingo ya kizazi ya mwanamke na pia kukumbwa na tatizo hili la miscarriage au kuharibika kwa mimba.

⬇️4.Chanzo kingine kikubwa ni magonjwa ya zinaa {sexually transmitted diseases}
magonjwa kama gonorrhea, kaswende mara nyingi sana huathili mfumo wa uzazi wa mwanamke na hasa  kwenye mji wa mimba na kuufanya kuwa legevu na hata ujauzito unapotunga basi huweza kutoka kwa haraka zaidi na hivyo kusababisha tatizo hili la kutoka kwa mimba {Miscarriage}.
⬇️5.Chanzo kingine cha mimba kuharibika ni tatizo la kisukari kwa mwanamke.

Hii nayo huchangia kwa kiasi kikubwa sana kuharibika kwa mimba na mtu ambaye hafanyi uangalizi wa karibu wa tatizo la sukari basi husababisha glucose isitumike kama energy na hivyo kuleta madhara katika kizazi hasa ujauzito.
⬇️6.kuvurugika kwa homoni

Kwa mfano hormone ya progesterone mara nyingi hufanya ile kazi ya kutunza mimba iendelee kukuwa, na kama kunatokea kwa hormon imbalance au kuvurugika kwa homoni hii basi mara nyingi tatizo hili la mimba kuharibika hutokea.
DALILI ZA KUHARIBIKA KWA MIMBA (Miscarriage)
🔔🔔Dalili kubwa kabisa ya kwanza ni damu nyepesi kutoka kwa mwanamke mwenye mimba ndani ya wiki 28 Toka apate Mimba.
🔔🔔Dalili kubwa ya pili ni mwanamke kutokwa na damu yenye mabonge mabonge na inakuwa nzito.
🔔🔔Dalili nyingine kubwa ni uchovu na maumivu makali ya kiuno na mgongo {miscarriage}.
🔔🔔 Maumivu makali ya tumbo, yakiambatana na maumivu ya kiuno pamoja na kutokwa na damu nyepesi au nzito basi ujue ujauzito wako uko kwenye hatari ya kutoka, ni vizuri kwenda  kituo  cha afya kilicho karibu nawe.

No comments:

Post a Comment