Monday, March 23, 2020

FAIDA 10 ZA KUNYONYESHA ZITAKAZO KUSHANGAZA

JE  WAJUA FAIDA ZA KUNYONYESHA KWA MAMA NA MTOTO??
Kuna faida kubwa anazo zipata mama na mtoto pia pindi akinyonyesha,faida kubwa kabisa ni hizi hapa;
Faida kwa mtoto:
🍎🍎• Humpatia virutubisho (viini lishe) vyote anavyohitaji kwa uwiano ulio sahihi kwa ukuaji na maendeleo yake;
🍎🍎• Humpatia kinga dhidi ya maradhi mbalimbali kama kuharisha, magonjwa ya njia ya hewa na masikio;
🍎🍎• Humwezesha mtoto kukua kimwili na kiakili kikamilifu;
🍎🍎• Huleta uhusiano mzuri na wa karibu kati ya mama na mtoto;(Bond of love)
🍎🍎• Watoto walionyonya maziwa ya mama huwa na mwenendo mzuri pamoja na akili ukilinganisha na wale wasionyonya maziwa ya mama.
🍎🍎• Maziwa ya mama humeng’enywa (huyeyushwa) kwa urahisi tumboni mwa
mtoto na hivyo kutumiwa na mwili kwa ufanisi.

⬇️⬇️🎯Faida kwa mama:🌍🌍

Huchangia katika kulinda afya ya mama kwa njia mbalimbali kama zifuatazo:
🌺🌺• Mama anaponyonyesha mara baada ya kujifungua husaidia tumbo la uzazi kurudi katika hali ya kawaida mapema.(hukuepusha na KITAMBI)
🌺🌺husaidia kupunguza damu kutoka
hivyo kuzuia upungufu wa wekundu wa damu (upungufu wa damu);
🌺🌺• Hupunguza uwezekano wa kupata ujauzito katika miezi sita ya mwanzo kama mama atamnyonyesha mtoto maziwa yake tu mara nyingi kwa siku na pia kama hajapata hedhi;(inamsaidia mama kupanga Uzazi miezi 6 ya mwanzoni)
🌺🌺• Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya mfuko wa uzazi, na matiti;
🌺🌺• Hujenga uhusiano wa karibu kati ya mama na mtoto;
🌺🌺•  kunyonyesha husaidia kumrudishia mama umbile lake la kawaida kwa kupunguza uzito akiwa ananyonyesha.
🌺🌺maziwa ya mama Ni safi na salama, hupatikana muda wote katika joto sahihi kwa mtoto na hayahitaji matayarisho;
🌺🌺• Gharama yake ni ndogo ukilinganisha na maziwa mbadala;
🌺🌺• Hayaleti matatizo ya mzio (“allergies”) kama pumu (asthma ) na magonjwa yangozi;

✍️✍️Mtoto aanze kunyonyeshwa maziwa ya mama yake mara tu anapozaliwa bila kumchanganyia na vyakula vingine Hadi atakapofika miezi sita ,au kama mama atapata Ushauri toka kwa doctor ili amchanganyie chakula Mtoto wake.

No comments:

Post a Comment