Friday, March 27, 2020

FANYE HIVI ILI UKE USITOE HARUFU MBAYA.ITAKUSAIDIA SANA.


☑️Fanya hivi  kujiepusha na harufu mbaya sehemu za siri kwa mdada?๐ŸŒบ
✍️✍️ HARUFU mbaya inaweza ikawa kero kubwa wakati wa Kushiriki TENDO la ndoa na kufanya mwenzi wako akose mood na wewe Tena,leo nimekuletea SURUHISHO la kumaliza shida hii.
๐ŸŒน๐ŸŒน-Epuka kusafisha uke kwa kuingiza kidole ukeni-Uke usafishwe kwa maji ya vuguvugu na sabuni ya kawaida ya kuogea (sio medicated soap), bila kuingiza kidole au kitu chochote ndani ya uke
๐ŸŒน๐ŸŒน-Epuka matumizi ya madawa ya antibiotics kwa muda mrefu bila ya kuambiwa na daktari-kwani dawa hizi zikitumika kwa muda mrefu na bila ushauri wa daktari husababisha mabadiliko katika bakteria wa kwenye uke na kupelekea magonjwa na harufu mbaya
๐ŸŒน๐ŸŒน-Vaa nguo za ndani za cotton
๐ŸŒน๐ŸŒน-Epuka nguo za kubana sana mwili,ili kuruhusu hewa ipite VIZURI
✍️✍️-Nguo ya ndani ianikwe nje; sehemu ambayo itapigwa na jua (na sio ndani ya chumba); au nguo za ndani zipigwe pasi kabla ya kuvaliwa,
✍️✍️-Unapokuwa kwenye siku zako zingatia usafi na kubadilisha pedi kama inavyotakiwa(mara 2-3 kwa siku)
๐ŸŒบ๐ŸŒบ-Epuka kutumia vyoo vya umma ambavyo ni vya kukaa,
๐ŸŒน๐ŸŒน-Jikinge na magonjwa ya zinaa,
✍️✍️-Epuka kuvaa nguo nyingi na/au nzito wakati wa kulala; vaa nguo nyepesi ambayo itaruhusu uke kupata hewa ya kutosha.
๐ŸŒบ-Jisafishe vizuri kila baada ya kumaliza haja ndogo,kwa Kutoka mbele kurudi nyama.
✍️✍️-Kitu kingine ambacho ni muhimu sana kufahamu, ikitokea ukaona kuwa uke wako unatoa harufu, kuuosha kwa maji mengi na sabuni nyingi mara nyingi, sio suluhisho bali unazidi kuleta matatizo zaidi kwa sababu unazidi kupunguza idadi ya bakteria wazuri, na kubadilisha hali ya utindikali wa uke na hivyo kukaribisha bakteria wabaya kwa wingi zaidi!!
-❤️๐Ÿ˜ kitu cha mwisho ambacho ni muhimu zaidi, ni kwetu wanaume, unapoona mwenzi wako ana tatizo hili, usimseme vibaya au kumkaripia au kumtukana; Unatakiwa kutambua kuwa huo ni ugonjwa na umsaidie kuweza kuonana na wataalamu wa Afya kwa ajili ya matibabu.
๐Ÿ˜๐Ÿ˜Hapo utakuwa MWANAUME imara.
#wote tuijenge Afya❤️❤️
❤️toa maoni yako hapo chini.

Monday, March 23, 2020

FAIDA 10 ZA KUNYONYESHA ZITAKAZO KUSHANGAZA

JE  WAJUA FAIDA ZA KUNYONYESHA KWA MAMA NA MTOTO??
Kuna faida kubwa anazo zipata mama na mtoto pia pindi akinyonyesha,faida kubwa kabisa ni hizi hapa;
Faida kwa mtoto:
๐ŸŽ๐ŸŽ• Humpatia virutubisho (viini lishe) vyote anavyohitaji kwa uwiano ulio sahihi kwa ukuaji na maendeleo yake;
๐ŸŽ๐ŸŽ• Humpatia kinga dhidi ya maradhi mbalimbali kama kuharisha, magonjwa ya njia ya hewa na masikio;
๐ŸŽ๐ŸŽ• Humwezesha mtoto kukua kimwili na kiakili kikamilifu;
๐ŸŽ๐ŸŽ• Huleta uhusiano mzuri na wa karibu kati ya mama na mtoto;(Bond of love)
๐ŸŽ๐ŸŽ• Watoto walionyonya maziwa ya mama huwa na mwenendo mzuri pamoja na akili ukilinganisha na wale wasionyonya maziwa ya mama.
๐ŸŽ๐ŸŽ• Maziwa ya mama humeng’enywa (huyeyushwa) kwa urahisi tumboni mwa
mtoto na hivyo kutumiwa na mwili kwa ufanisi.

⬇️⬇️๐ŸŽฏFaida kwa mama:๐ŸŒ๐ŸŒ

Huchangia katika kulinda afya ya mama kwa njia mbalimbali kama zifuatazo:
๐ŸŒบ๐ŸŒบ• Mama anaponyonyesha mara baada ya kujifungua husaidia tumbo la uzazi kurudi katika hali ya kawaida mapema.(hukuepusha na KITAMBI)
๐ŸŒบ๐ŸŒบhusaidia kupunguza damu kutoka
hivyo kuzuia upungufu wa wekundu wa damu (upungufu wa damu);
๐ŸŒบ๐ŸŒบ• Hupunguza uwezekano wa kupata ujauzito katika miezi sita ya mwanzo kama mama atamnyonyesha mtoto maziwa yake tu mara nyingi kwa siku na pia kama hajapata hedhi;(inamsaidia mama kupanga Uzazi miezi 6 ya mwanzoni)
๐ŸŒบ๐ŸŒบ• Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya mfuko wa uzazi, na matiti;
๐ŸŒบ๐ŸŒบ• Hujenga uhusiano wa karibu kati ya mama na mtoto;
๐ŸŒบ๐ŸŒบ•  kunyonyesha husaidia kumrudishia mama umbile lake la kawaida kwa kupunguza uzito akiwa ananyonyesha.
๐ŸŒบ๐ŸŒบmaziwa ya mama Ni safi na salama, hupatikana muda wote katika joto sahihi kwa mtoto na hayahitaji matayarisho;
๐ŸŒบ๐ŸŒบ• Gharama yake ni ndogo ukilinganisha na maziwa mbadala;
๐ŸŒบ๐ŸŒบ• Hayaleti matatizo ya mzio (“allergies”) kama pumu (asthma ) na magonjwa yangozi;

✍️✍️Mtoto aanze kunyonyeshwa maziwa ya mama yake mara tu anapozaliwa bila kumchanganyia na vyakula vingine Hadi atakapofika miezi sita ,au kama mama atapata Ushauri toka kwa doctor ili amchanganyie chakula Mtoto wake.

ACHA KUFANYA MAPENZI UKIFIKIA HATUA HII KWENYE UJAUZITO

๐Ÿ””Je, ni wakati gani mwanamke mjamzito anatakiwa kuacha kufanya mapenzi?๐ŸŽ

Ijapokuwa wapo wanawake wengi ambao wanaweza kabisa kuendelea kufurahia kufanywa hadi siku wanakwenda kujifungua na kufanya Mapenzi KIPINDI Cha UJAUZITO hakuna TATIZO lolote kwa Mtoto /mama , kuna baadhi ya nyakati mshauri wako wa afya anaweza kukushauri kuacha ngono kutokana na moja au zote kati ya yafuatayo:
1️⃣umekuwa na tatizo la kujifungua kabla ya muda muafaka kabla ya ujauzito ulio nao.
2️⃣tatizo la kutokwa na damu kwenye uke.
3️⃣umekuwa ukitokwa na ute fulani ambao kitaalamu tunaita kwa jina la "amniotic fluid"
4️⃣umekuwa na tatizo kwenye mlango wa uzazi, ambalo kitaalamu linajulikana kama cervical incompetence.
5️⃣kondo la nyuma limesambaa na kuziba kabisa mlango wa uzazi na kuanza kujitokeza kwa nje (placenta previa)
✍️✍️na SABABU nyingine doctor atakazokuona nazo ataweza kukushauri usiendelee kufanya Ngono.
๐ŸŽ๐ŸŽ๐ŸŽ online clinic⚕️⚕️

SABABU NA DALILI ZA MIMBA KUTOKA YENYEWE

[๐ŸŽฏ JE WAJUA VISABABISHI VYA  KUHARIBIKA KWA MIMBA๐ŸŒน๐ŸŒน {Miscarriage}?
Kuharibika kwa mimba ni janga kwa wanawake wengi siku hizi,na kama bado unajiuliza nini sababu za mimba kutoka,soma hizi hapa utaelewa;
⬇️1.Chromosome abnormalities,
mimba nyingi ambazo huharibika hadi wiki ya ishirini husababishwa na tatizo hili la chromosomes, na chromosomes huwa zinabeba genes ambazo huyatambulisha maumbile ya mwanadamu kwa nje, yaani jinsia yake, ngozi yake itakuaje, macho yake na vitu vingine vingi nisingependa tuingie ndani sana lakini matatizo haya ya chromosomes huchangia sana kuharibika kwa mimba.

⬇️2.Maambukizi katika mji wa uzazi wa mwanamke {Infections}
kuna kitu kinaitwa Pelvic Inflammatory Diseases {PID} yaani kuvimba kwa kuta za mji wa mimba au kuvimba kwa mirija ya uzazi nayo pia huchangia sana kuharibika kwa mimba kwa mwanamke, lakini pia Candida au fangasi nazo pia huchangia sana kuharibika kwa mimba.

⬇️3.Chanzo kingine kikubwa ni utoaji wa mimba
Utoaji wa mimba wa mimba za mara kwa mara, wanawakie au wasichana wenye tabia ya kutoa mimba moja au mbili au tatu basi nao pia hukutwa na tatizo hili la kuharibika kwa mimba kwani uingizaji wa vyuma ndani huweza kuharibu shingo ya kizazi ya mwanamke na pia kukumbwa na tatizo hili la miscarriage au kuharibika kwa mimba.

⬇️4.Chanzo kingine kikubwa ni magonjwa ya zinaa {sexually transmitted diseases}
magonjwa kama gonorrhea, kaswende mara nyingi sana huathili mfumo wa uzazi wa mwanamke na hasa  kwenye mji wa mimba na kuufanya kuwa legevu na hata ujauzito unapotunga basi huweza kutoka kwa haraka zaidi na hivyo kusababisha tatizo hili la kutoka kwa mimba {Miscarriage}.
⬇️5.Chanzo kingine cha mimba kuharibika ni tatizo la kisukari kwa mwanamke.

Hii nayo huchangia kwa kiasi kikubwa sana kuharibika kwa mimba na mtu ambaye hafanyi uangalizi wa karibu wa tatizo la sukari basi husababisha glucose isitumike kama energy na hivyo kuleta madhara katika kizazi hasa ujauzito.
⬇️6.kuvurugika kwa homoni

Kwa mfano hormone ya progesterone mara nyingi hufanya ile kazi ya kutunza mimba iendelee kukuwa, na kama kunatokea kwa hormon imbalance au kuvurugika kwa homoni hii basi mara nyingi tatizo hili la mimba kuharibika hutokea.
DALILI ZA KUHARIBIKA KWA MIMBA (Miscarriage)
๐Ÿ””๐Ÿ””Dalili kubwa kabisa ya kwanza ni damu nyepesi kutoka kwa mwanamke mwenye mimba ndani ya wiki 28 Toka apate Mimba.
๐Ÿ””๐Ÿ””Dalili kubwa ya pili ni mwanamke kutokwa na damu yenye mabonge mabonge na inakuwa nzito.
๐Ÿ””๐Ÿ””Dalili nyingine kubwa ni uchovu na maumivu makali ya kiuno na mgongo {miscarriage}.
๐Ÿ””๐Ÿ”” Maumivu makali ya tumbo, yakiambatana na maumivu ya kiuno pamoja na kutokwa na damu nyepesi au nzito basi ujue ujauzito wako uko kwenye hatari ya kutoka, ni vizuri kwenda  kituo  cha afya kilicho karibu nawe.

FAIDA 10 ZA KUFANYA MAPENZI UKIWA MJAMZITO

Kuna watu wamekua wakiuliza mara kwa mara kama inaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa mpaka umri gani wa mimba au ni sahihi kufanya tendo la ndoa kipindi cha ujauzito?

✍️Mwanamke akiwa na mimba anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa hata kama anatarajia kuzaa kesho yake, hakuna tatizo lolote linalomzuia kufanya hivyo, baadhi ya wanawake wamekua wazito sana kufanya hivyo kwa kua na sababu mbalimbali za kujitetea bila kujua kwamba wanazikosa faida hizi ambazo ni muhumu kiafya.faida zenyewe ni kama zifuatazo:

1️⃣Husaidia uchungu mzuri na kupona mapema; kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa huambatana na kubana kwa misuli ya nyonga hii husaidia kuweka imara misuli ya nyonga ambayo ni muhimu sana wakati wa kusukuma mtoto na baada ya kuzaa kwani misuli hii ikiwa legevu mwanamke huweza kushindwa kuzaa kwa njia ya kawaida na hata baada ya kuzaa huweza kushindwa kuzuia mkojo usitoke wenyewe au kuvuja damu kwa muda mrefu.
2️⃣Hupunguza kwenda ovyo kukojoa au kujikojolea; wakati wa ujauzito mtoto anapozidi kua mkubwa anazidi kukandamiza kibovu cha mkojo, hii humfanya mama aende chooni kukojoa mara kwa mara na wakati mwingine hata akipiga chafya au kukohoa basi mkojo unaweza kutoka wenyewe. tendo la ndoa huibana misuli ya nyonga na kuzuia hali hii.
3️⃣Huzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba; tafiti zinaonyesha kwamba aina ya protini inayopatikana kwenye mbegu za mwanaume huongeza kinga ya mwili na kuzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba ambacho kinaua wanawake wengi sana.

4️⃣Hutibu tatizo la kufika kileleni kwa shida; kipindi cha ujauzito chuchu za mwanamke na kinembe chake huvimba na kuongezeka hisia mara dufu huku kiwango cha homoni za oestrogen kikiwa juu sana, hii humfanya kufika kileleni kirahisi sana kuliko mwanzoni.5️⃣Huwapa uwezo wa kujiamini; kipindi cha ujauzito mwanamke hua anapata hofu sana na kutojiamini na mwili wake, hua na wasiwasi kwamba mwili wake unaharibika hivyo kitendo cha mwanaume wake kuendelea kushiriki naye tendo la ndoa humpa kujiamini kwamba mwili wake bado uko kwenye hali nzuri na anapendwa.kipindi Cha UJAUZITO MWANAMKE anakuwa mtamu ZAIDI.

6️⃣Hupunguza msongo wa mawazo; kipindi cha ujauzito wanawake wengi huwaza sana kuhusu kesho yao...je swala la uchumi litakuaje? mwili wangu utakuaje? je nitapata jinsia nayotegemea? na kadhalika.. tendo la ndoa hutoa homoni ya upendo kwa jina la oxytocin(hormone of love), homoni hii hupunguza mawazo na kumpa amani mjamzito.

7️⃣Huongeza upendo na mshikamano kati ya wapenzi; katika hali ya kawaida wanandoa wakikwazana wanaweza wakapatana kwa kushiriki tendo la ndoa tu, amani na upendo kipindi hiki ni muhimu sana kwani kuna mtoto anakuja ambaye anatakiwa kuzaliwa huku baba na mama wakiwa wanapatana na kupendana.

8️⃣Hukuandaa na uchungu; ukishiriki  TENDO LA ndoa wakati wa tarehe zilizokadiriwa zimefika unapata homoni moja kutoka kwenye mbegu za mwanaume kwa jina la prostglandin, homoni hii huivisha mlango wa uzazi na kuanza kufunguka taratibu kujiandaa na uchungu.

9️⃣Hutibu tatizo la kukosa usingizi; wanawake wengi wajawazito hua na dalili mbalimbali za maumivu na kuumwa sehemu tofauti za mwili na msongo wa mawazo, hii huweza kuwakosesha usingizi kabisa..tendo la ndoa huweza kuwapa usingizi mzuri Sana pale watakapofikishwa kileleni.

๐Ÿ”ŸHupunguza presha ya damu; kipindi cha tendo la ndoa presha ya damu hushuka kwenye kiwango kizuri sana, hii ni muhimu sana kwa wanawake wenye hatari ya kupata kifafa cha mimba kama wanene sana, wenye kisukari au wenye historia za ugonjwa wa presha kwenye koo zao.

๐ŸŒน๐ŸŽHakikisha unatumia staili za tendo la ndoa ambazo hazimuumizi mtoto na mama yaani hakikisha haulilalii tumbo hasa mimba ikiwa kubwa,
๐Ÿ›Œ๐Ÿ‘Œ kuna staili muhimu kipindi hiki kama kuangalia upande mmoja, mwanamke kuja juu, au mwanamke kuinama
๐ŸŽ✍️ online clinic⚕️ MwanaApp ♥️